🍹Morning Rise Up🍹
✍🏽 *IMANI HII NDIYO YA KUIGA*.
_Wakati ule wa masika chakula kilikuwa haba ,hatukuwa hata chakula cha kutosha kwenye ghala .Ghalani kulikuwa na kiasi kidogo cha maharage kilichokuwa kimebaki .Kwa vile ilikuwa ni wakati wa masika ,Mama alituambia kuwa maharage yaliyobaki yalikuwa ni ya kupanda na si kwa ajili ya chakula .Tulipomuuliza tutakula nini mama alisema "Sikilizeni wanangu ,tutakula hata kisamvu au hata karanga za kupikwa lakini lazima tupande maharage haya tuyapande kwa ajili ya kupata chakula cha mwakani ,tukishindwa kufanya hivyo mwakani hatutakuwa na chakula hivyo basi hatuwezi kuacha kupanda maharage haya yaliyobaki kwa njaa ya mwezi mmoja wakati tukipanda haya baada ya miezi miwili tu tutaanza kufaidi .Ninajua mtaumia sana wanangu lakini hali yetu ya maisha mnaijua ,hatuna uwezo wa kununua kila kitu inabidi tulime ili kupunguza gharama za maisha maana hela ya shule yenu itatoka humu kwenye kilimo hiki hiki_
_Wakati huo mimi na wadogo zangu hatukumuelewa mama maana hatukuwa tunapenda tupitie shida ya kula ugali kwa karanga za kuchemshwa au kisamvu wakati maharage yalikuwa Ghalani lakini baadae maharage yale yalivyopandwa na tukianza kuvuna ndipo tulipokuwwa tunajua nini mama alikuwa anamanisha_
*TAFAKURI & FUNDISHO*
```1. Maisha kuelekea kule unakokutaka yanahitaji *Imani* ,Lakini Imani hiyo iambatane na Udhubutu .Watu wengi huwa wanaweza kuwa na Imani lakini Imani hiyo ikakosa udhubutu .Angalia Mkulima alivyo na Imani kubwa ya kuzika mbegu zake adhini sehemu ambako hata hazioni hata kama hana chakula cha kutosha lakini huamini kuwa mbegu zile anazozika ardhini muda si mrefu zitazaa na kupata faida kubwa kuliko angekula zile mbegu kwa njaa ya siku moja huku akikaribisha njaa ya mwaka mzima .Huu ni udhubutu usio na kifani ambao watu wengi huwa hawawezi kufanya katika maisha..Kujua kuwa mbegu zitazaa nyingi zaidi ni IMANI lakini hatua ya Kuzika mbegu ardhini ni UTHUBUTU .Kumbuka Imani bila matendo Imekufa .Watu wengi wanaamini lakini huwa hawadhubutu .
2. Kuna watu wakisikia unataka kuwekeza sehemu fulani kwa gharama na huna hela za kutosha watakwambia subiri ujipange upate hela kubwa maana ukiweka hela hiyo uliyonayo wanakwambia maisha yako yatakuwa magumu na unaweza kushindwa kuishi .Angalia mkulima hupanda mbegu zake bila majuto hata kama hana chakula .Huamini kuwa kwa kupanda mbegu ndiko kufanikiwa kupata zaidi .Yuko tayari kula chochote kinachopatikana kwa wakati huo akijua tabu atakayopitia ni ya Muda mfupi .Sikia unapoamua kufanya jambo acha kujihurumia acha kuwapa nafasi watu wakuhurumie wakati hata hawajui nini faida utakayoipat```
No comments