Select Menu

Slider

Powered by Blogger.

Music

Health

Sports

News

Photos

Documentary

Video

» » ZIJUE SABABU ZINAZOKUFANYA USHINDWE KUANZA WAZO LAKO . .....
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

ZIJUE SABABU ZINAZOKUFANYA USHINDWE KUANZA WAZO LAKO...

Usiku mwangavu ulikuwa unaingia. Katika hotel moja kulikuwa na maongezi ya vijana watatu wenye ndoto kubwa na walikuwa na mawazo mazuri sana. Lakini shida kubwa ilikuwa ni namna gani ya kuweza kuifanya ndoto iwe halisi. Usiwe na usiku mrefu wa ndoto amka uanze kuitenda.

Katika kundi la watu 10 watu 9 kati yao wanaota ndoto. Ingewezekana kutekelezwa kwa kila ndoto na kila wazo dunia ingekuwa tofauti na jinsi ilivyo.

Hebu fikiri juu ya miradi mikubwa ambayo mpaka sasa ipo katika mawazo, vitabu ambavyo mpaka sasa havijawekwa katika kurasa, ule ujumbe mzuri ambao mpaka sasa haujahubiriwa, na kiongozi mzuri ambaye mpaka sasa hajaweza kusimama katika nafasi yake....yote haya ni mawazo. Utajiri uliopo katika ndoto na mawazo ni mkubwa kuliko hazina zote katika migodi, bahari na maliasili zote...

Lakini kwa nini watu hawachukui hatua ya kuanza??

Zipo sababu kadhaa nitazijadili kwa kifupi ili uweze kupatwa mwanga na ikiwezekana uthubutu kuanza..

1. Hofu. Kwa kawaida watu wanahofu kwa mambo yanayofikirika tu, mambo ambayo siyo kweli. Kwa mfano watu huogopa giza kwa kuhofia kitu ambacho hawakijui lakini hujiumba na kuwa kweli mawazoni mwao wenyewe.
2. Kutokueleweka. Uwezo na ubora wa wazo unatofautiana. Kwa mfano mtu aliyejizoeza kutekeleza mawazo yake uwezo wa kuchuja na kupembua mawazo yake ni bora zaidi. Wazo linapokua na maana zaidi ya moja akili haitaweza kulitekeleza kirahisi ni lazima kutakuwa na mvutano.

3. Incompatibility. Hii ni aina ya mawazo ambayo hayawezi kuchukuliana na hali au na kazi yako ya sasa. Kwa mfano mimi ni mwajiriwa na ninataka kufanya kitu kitakacho hitaji niache kazi yangu ya sasa. Kuanza kutekeleza wazo la aina hii ni vigumu. Inawezekana lakini itahitajika nguvu kubwa kutokea nje.

4. Urahisi wa kutekeleza. Hujaelewa bado kama hauwezi kurahisisha. Siri kubwa ya majiniasi ni kufanya mambo magumu yawe rahisi na yanayotekelezeka. Wazo kuwa gumu na kubwa mno linafanya akili iwe na kusitasita kutekeleza.

Kwa sababu hii ikiwa unataka kuchukua wazo la aina yoyote ile jifunze kuliumba wazo katika namna rahisi ambayo unaweza kuiandika na kuichora. Na usahihi wa mawazo huonekana pale unapomshirikisha mwingine na akaweza kulielewa kirahisi tu. Ni mhimu kuwa na watu mhimu ambao wanaweza kukushauri ili uweze kupima mawazo yako. Kumbuka katika mashauri ya wengi mipango hutimia. Na mpango ni wazo lililowekwa katika maandishi.

About Arusha99

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply