Select Menu

Slider

Powered by Blogger.

Music

Health

Sports

News

Photos

Documentary

Video

» » EPUKA UTAPELI KATIKA SIMU KWA KS MA KISA HICHI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

UTAPELI KTK SIMU

Uungwana una gharama zake.

Dakika chache zilizopita amenipigia mtu simu.  Ametumia namba 0764882284, akajitambulisha anaitwa Paul akipiga simu kutoka Vodacom Huduma kwa Wateja.  Akaniambia kuwa kuna mtu amepiga simu kuwa amenitumia pesa kupitia Mpesa kwa makosa.  Nikamwambia kuwa sijaona pesa yoyote ikiingia kwenye simu yangu.

Akaniambia kuwa wakati mwingine sms huchelewa kuingia kwa sababu za kimtandao.  Kwa kuwa kila siku ninatumia huduma hiyo, akili yangu inayasadiki maelezo yake.

Akaniuliza kama ninakumbuka salio langu la mwisho.  Kwa kuwa ninatumia sana hii huduma, ninafahamu salio langu.  Ukizingatia tayari akili yangu iliwaza kuwa ninazungumza na mfanyakazi wa Vodacom, sikusita kumtajia kuwa kwenye akaunti yangu kuna 42,570/=

Akaniambia kama sms haijaingia nisubiri atanipigia pindi itakapoingia.

Wakati namaliza tu kuongea naye, napokea sms (kwa haraka haraka niliiona kama ya Mpesa) ikinionesha kuwa nimepokea kiasi cha shilingi 40,000/= kutoka namba 0759526921 iliyosajiliwa kwa jina la Daniel Oswald.

Wakati tu namaliza kuisoma hiyo sms napokea simu kwa yule bwana aliyejitambulisha kuwa anaitwa Paul akipiga simu kutoka Vodacom.  Nikidhani ninazungumza na mtu wa Vodacom, na kwa uungwana kwa kuwa nimeona watu wengi wakipoteza pesa nyingi kwa kutuma kimakosa, ninamjibu kuwa nimeona hiyo text kuwa 40,000/= imeingia kwenye simu yangu.

Bwana Paul, kama alivyojitambulisha, akaniambia kwa kuwa system ya Vodacom ipo slow anaomba nimsaidie kuirudisha hiyo pesa kwenye namba 0759526921.  Nikamwambia sawa hakuna tatizo nitafanya hivyo. Akaniambia nirudishe 39,000/= ili nisikatwe mie ada ya muamala.

Kwa kuwa akili yangu ilizingatia kuwa kweli kuna pesa imeingia, nilipokata tu simu sikurudi tena kwenye sms.  Nikapiga * 150*00#.  Nikatuma pesa kwenye hiyo namba ambayo nilikuwa tayari nimeinakili kwenye notebook yangu.  Tena wakati natuma nilikuwa nikimwambia mtu niliyekuwa naye kuwa huwa naona huruma sana mtu akikosea kutuma pesa.  Huwezi jua wakati mwingine ana shida kiasi gani.  Wacha nifanye hima kumrejeshea.

Mpesa waliponiletea sms ya kukamilika kwa muamala naona salio langu limeshuka hadi elfu tatu na ushei.

Ndipo akili ikachangamka.  Nikaenda kwenye sms ya nyuma na kugundua nimetapeliwa.  Nikapiga Vodacom huduma kwa wateja.  Nilipotoa maelezo, wakaniambia hiyo pesa tayari imekwishatolewa kwenye simu ya mhusika.  Kwamba hawawezi kuwa na namna ya kunirejeshea.  Chini ya dakika tatu ujue.

Nikamtumia text huyo bwana Paul (kama alivyojitambulisha) kuwa namshukuru sana kwa kunitapeli lakini 39,000/= itamwongezea tu umasikini, zaidi, umasikini wa fikra.

Halafu nikacheka tu.  Nami leo nimepatikana.  Ama kweli, ndege mjanja, lake tundu bovu.

Kwa nini nimetumia muda wangu kuyaandika haya?  Sitaki nawe utapeliwe.  Angalau, isiwe kizembe kama nilivyofanya mie.

Mchana mwema.

Fadhy Mtanga,
Mbeya.
Alhamisi, Septemba Mosi, 2016.
SHARE NA WENGINE WASIUMIZWE

About Arusha99

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply