UTAPELI KTK SIMU
Uungwana una gharama zake.
Dakika chache zilizopita amenipigia mtu simu. Ametumia namba 0764882284, akajitambulisha anaitwa Paul akipiga simu kutoka Vodacom Huduma kwa Wateja. Akaniambia kuwa kuna mtu amepiga simu kuwa amenitumia pesa kupitia Mpesa kwa makosa. Nikamwambia kuwa sijaona pesa yoyote ikiingia kwenye simu yangu.
Akaniambia kuwa wakati mwingine sms huchelewa kuingia kwa sababu za kimtandao. Kwa kuwa kila siku ninatumia huduma hiyo, akili yangu inayasadiki maelezo yake.
Akaniuliza kama ninakumbuka salio langu la mwisho. Kwa kuwa ninatumia sana hii huduma, ninafahamu salio langu. Ukizingatia tayari akili yangu iliwaza kuwa ninazungumza na mfanyakazi wa Vodacom, sikusita kumtajia kuwa kwenye akaunti yangu kuna 42,570/=
Akaniambia kama sms haijaingia nisubiri atanipigia pindi itakapoingia.
Wakati namaliza tu kuongea naye, napokea sms (kwa haraka haraka niliiona kama ya Mpesa) ikinionesha kuwa nimepokea kiasi cha shilingi 40,000/= kutoka namba 0759526921 iliyosajiliwa kwa jina la Daniel Oswald.
Wakati tu namaliza kuisoma hiyo sms napokea simu kwa yule bwana aliyejitambulisha kuwa anaitwa Paul akipiga simu kutoka Vodacom. Nikidhani ninazungumza na mtu wa Vodacom, na kwa uungwana kwa kuwa nimeona watu wengi wakipoteza pesa nyingi kwa kutuma kimakosa, ninamjibu kuwa nimeona hiyo text kuwa 40,000/= imeingia kwenye simu yangu.
Bwana Paul, kama alivyojitambulisha, akaniambia kwa kuwa system ya Vodacom ipo slow anaomba nimsaidie kuirudisha hiyo pesa kwenye namba 0759526921. Nikamwambia sawa hakuna tatizo nitafanya hivyo. Akaniambia nirudishe 39,000/= ili nisikatwe mie ada ya muamala.
Kwa kuwa akili yangu ilizingatia kuwa kweli kuna pesa imeingia, nilipokata tu simu sikurudi tena kwenye sms. Nikapiga * 150*00#. Nikatuma pesa kwenye hiyo namba ambayo nilikuwa tayari nimeinakili kwenye notebook yangu. Tena wakati natuma nilikuwa nikimwambia mtu niliyekuwa naye kuwa huwa naona huruma sana mtu akikosea kutuma pesa. Huwezi jua wakati mwingine ana shida kiasi gani. Wacha nifanye hima kumrejeshea.
Mpesa waliponiletea sms ya kukamilika kwa muamala naona salio langu limeshuka hadi elfu tatu na ushei.
Ndipo akili ikachangamka. Nikaenda kwenye sms ya nyuma na kugundua nimetapeliwa. Nikapiga Vodacom huduma kwa wateja. Nilipotoa maelezo, wakaniambia hiyo pesa tayari imekwishatolewa kwenye simu ya mhusika. Kwamba hawawezi kuwa na namna ya kunirejeshea. Chini ya dakika tatu ujue.
Nikamtumia text huyo bwana Paul (kama alivyojitambulisha) kuwa namshukuru sana kwa kunitapeli lakini 39,000/= itamwongezea tu umasikini, zaidi, umasikini wa fikra.
Halafu nikacheka tu. Nami leo nimepatikana. Ama kweli, ndege mjanja, lake tundu bovu.
Kwa nini nimetumia muda wangu kuyaandika haya? Sitaki nawe utapeliwe. Angalau, isiwe kizembe kama nilivyofanya mie.
Mchana mwema.
Fadhy Mtanga,
Mbeya.
Alhamisi, Septemba Mosi, 2016.
SHARE NA WENGINE WASIUMIZWE
social
Tafadhali Share na marafiki story hii🍹Morning Rise Up🍹
✏```HUPASWI KULA KILA KITU SAFARINI```
_Tulipokuwa stendi ya magari kabla ya kutoka *Ubungo* ,ndugu *Mla vyote* alinunua maji akijua yatamsaidia njiani .Tulivyokuwa tukiendelea na safari ndugu huyu alikuwa anatamani kununua kila kitu ambacho alikuwa analetewa dirishani asijue kama yuko safarini_
_Tulivyofika *Morogoro* mla vyote *alinunua chips* ili zimsaidie njiani kabla ya kufika sehemu ambapo angepata chakula cha mchana maana tulikuwa tuko mbali na Kitonga ambayo ilikuwa ndiyo g&sehemu ambapo tungepata Chakula._
_Alivyokula zile chips ndugu huyu hakujua kuwa zile chips zilikuwa zimechacha na mara tu baada ya kula chips tumbo lake likaanza kusumbua na safari yake ikaanza kuwa mbaya .Hakuwa tena ana furaha ya safari ile kwa kuwa kila muda tumbo la kuhara lilikuwa linamsumbua. *Loo!* Mla vyote Alipata shida sana na hasa ukizingatia kuwa basi lilikuwa halina choo Nilimuonea huruma sana lakini sikuwa na jinsi ya kumsaidia zaidi ya kumpa pole na kufanya jitahada za kutafuta namna ya kutuliza tumbo lake lilokuwa likimuuma sana_
_Mla vyote aliniambia kuwa sasa amaejifunza kutokurupuka kula vitu njiani wakati anasafari kwa kuwa safari siyo sherehe ._
*TAFAKURI*
📝```Maisha ni safari ndefu inayohitaji umakini mkubwa sana .Wakati uko njiani utakutana na watu wengi ambao wanaweza kukudhuru na usiendelee na safari au kutofurahia safari yako.Watu wa namna hii unapaswa kukaa nao mbali huku ukiweka pamba masikioni kutosikiliza yale wanayoyasema .
📝Maneno ya kukatisha tamaa ni moja ya vyakula vyenye sumu na vilivyochacha ambavyo vitasababisha uone safari yako kuwa chungu .Njiani wakati unaendelea na hatua za ndoto yako utakutana na mambo ambayo unaweza kufikiri kuwa vitakusaidia kukufikisha kwenye hatma ya ndoto zako kumbe vinaua ndoto zako.
📝Achana kabisa na vitu ambavyo havina tija katika safari yako ya kufika pale unapotaka kufika .Sikia siyo lazima kuzingatia kila ushauri unaopewa na watu maana unaweza kukudhuru kama Mla vyote aliyodhurika na chips alizokuwa amenunua akidhani kama zingemsaidia .
📝Iko hivi Mpendwa,utakaporuhusu kila kitu kuingia masikioni mwako na kwenye ubongo wako kuna wakati ubongo wako utajaa sumu na utaona kila kitu hakiwezekani .
Wakati mwingine nikiwa nafundisha hatua tano za kufikia mafanikio kwenye Kijana Jithamini niliwaambia kuwa ubongo wa mwanadamu ni kama glasi yenye maji ambayo maji hayo mtu akiweka sukari maji hayo yatakuwa matamu ,lakini maji hayo hayo mtu akiweka sumu ,ukinywa utakufa```
Recent Comments