Select Menu

Slider

Powered by Blogger.

Music

Health

Sports

News

Photos

Documentary

Video

» » AJALI HAIKUKATISHA NDOTO YA WAKONTA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

🍹Morning Rise Up🍹

✍🏽```AJALI HAIKUKATISHA NDOTO YA WAKONTA👇👇 ```
Jana nikiwa nasikiliza taarifa ya habari *TBC1* katika kipindi cha *HADUBINI* nilikutana na jambo lilonisikitisha sana.Ni jambo lilomkuta Wakonta Kapunda ambaye alikuwa akisoma Masomo ya kidato cha sita mwaka 2012 katika shule ya sekondari ya wasichana ya Korogwe iliyoko mkoani Tanga .Kisa hiki ni cha kweli na iko hivi:

_Ilikuwa ni siku ya mahafari ya kumaliza kidato cha sita shule ya wasichana Korogwe *mwaka 2012*,kama ilivyo ada siku ya sherehe wanafunzi na hasa wahitimu hujawa na furaha tele  ndivyo ilivyokuwa kwa wahitimu siku hiyo akiwemo Wakonta._

_Basi wakati wa shamrashamra za huku na kule kabla ya sherehe kuanza rasmi ,wahitimu walikuwa wakizunguka huku na kule wakisalimiana na ndugu na marafiki waliokuwa wamefika kwenye sherehe hiyo .Wakonta naye alikuwa akipeana mkono wa pongezi na ndugu zake huku akiwa amejawa na furaha tele ya kumaliza masomo ya kidato cha sita._

_Wakati shamrashamra hizo zikiendelea na Wakonta akiwa anaenda huku na kule  ghafla mhitimu mmoja aliyekuwa akiendesha gari ambalo lilisemekana lilikuwa la mjomba wake alimgonga Wakonta na wakonta akaaumia sana huku shingo lake likivunjika na sehemu nyingi sana za mwili zikivunjika vibaya.Loo! Simanzi ,Vilio vilijaa na sherehe ile haikuwa sherehe tena kilio kikatawala kwa jambo lilokuwa limetokea na sherehe haikuweza kuendelea ,Wakonta akawa amekimbizwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matabibu_.

_Ashukuriwe *Mungu* kuwa hakuna aliyepoteza maisha ingawa Wakonta alivunjika sana na baada ya matibabu hakuwa tena anaweza kufanya chochote kwa kutumia mikono wala miguu akawa ni mtu wa kufanyiwa kila kitu kwa kuwa viungo vyote vilikuwa vimelemaa.Mama yake mzazi na baba yake mzazi ndio wanamsaidia kufanya kila kitu._

_Hata hivyo Wakonta anasema kuwa pamoja na kupata ajari mbaya sana iliyomlemaza viungo hakukata tamaa na ndoto yake .Wakonta anatumia ulimi wake kutumia *IPAD* kuingia mtandaoni na kutafuta *taarifa* hasa za uandishi wa Script za Movie maana ndoto yake ni kuwa mwandishi mkubwa wa kuandaa senima na amekuwa akiandika mara kwa mara huku akipata taarifa na maarifa kupitia mtandao wa Internet.Nilishuhudia jana kupitia *TBC 1* Wakonta akiwa anatumia ulimi kwa ufundi mkubwa sana kuandika script hizo ambapo ulimi hugusa vitufe vya IPAD na kuandika .Ni kitu ambacho unaweza usiamini lakinii ndivyo ilivyo kuwa hutumia ulimi kuandaa sinema hizo na tayari ana kikundi cha kuigiza ambaye yeye anategemewa huko kwao ama kweli hujafa hujaumbika_ .

_Wakonta sasa baada ya serikali kumsikia,waziri wa habari mheshimiwa Nape Nauye alifika kwao kwa ajili ya kumsaidia na hasa kukuza kipaji chake alichonacho_

*TAFAKURI*

```📝Maisha yetu yako mikononi mwa Mungu .Mshukuru Mungu kwa kuwa hai leo .Kesho yetu hatuijui ni bora sana tukaishi leo kwa kufanya makubwa sana kadri ya uwezo wetu .Wakonta hakujua kitakachompata siku ile ya sherehe .

📝Wakonta ametoa somo kubwa kwamba pamoja na kuwa viungo vyake vimelemaa hakubweteka na kuona kuwa ndoto zake haziwezekani na sasa kwa kutokuficha kipaji chake serikali imemuona .Yawezekana wewe ni mzima na pengine huna hata ulemavu lakini umeficha uwezo wako hata sielewi ni sababu ipi ya msingi .Hujajiuliza kwanini wanapata ajari wengine siyo wewe??? Mbona siku ile unasafiri ilipotokea ajari alikufa mwingine siyo wewe???? .Anza kufanya unayoweza kufanya bila kusingizia chochote maana kama ni kisingizio Wakonta angekaa asifanye chochote na watu wakamsaidia . ```

About Arusha99

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply