Select Menu

Slider

Powered by Blogger.

Music

Health

Sports

News

Photos

Documentary

Video

» » HUPASWI KULA KITU SAFARINI
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

🍹Morning Rise Up🍹

✏```HUPASWI KULA KILA KITU SAFARINI```

_Tulipokuwa stendi ya magari kabla ya kutoka *Ubungo* ,ndugu *Mla vyote* alinunua maji akijua yatamsaidia njiani .Tulivyokuwa tukiendelea na safari ndugu huyu alikuwa anatamani kununua kila kitu ambacho alikuwa analetewa dirishani asijue kama yuko safarini_

_Tulivyofika *Morogoro* mla vyote *alinunua chips* ili zimsaidie njiani  kabla ya kufika sehemu ambapo angepata chakula  cha mchana maana tulikuwa tuko mbali na Kitonga ambayo ilikuwa ndiyo g&sehemu ambapo tungepata Chakula._

_Alivyokula zile chips ndugu huyu hakujua kuwa zile chips zilikuwa zimechacha na mara tu baada ya kula chips tumbo lake likaanza kusumbua na safari yake ikaanza kuwa mbaya .Hakuwa tena ana furaha ya safari ile kwa kuwa kila muda tumbo la kuhara lilikuwa linamsumbua. *Loo!* Mla vyote Alipata shida sana na hasa ukizingatia kuwa basi lilikuwa halina choo Nilimuonea huruma sana lakini sikuwa na jinsi ya kumsaidia zaidi ya kumpa pole na kufanya jitahada za kutafuta namna ya kutuliza tumbo lake lilokuwa likimuuma sana_

_Mla vyote aliniambia kuwa sasa amaejifunza kutokurupuka kula vitu njiani wakati anasafari kwa kuwa safari siyo sherehe ._

*TAFAKURI*

📝```Maisha ni safari ndefu inayohitaji umakini mkubwa sana .Wakati uko njiani utakutana na watu wengi ambao wanaweza kukudhuru na usiendelee na safari  au kutofurahia safari yako.Watu wa namna hii unapaswa kukaa nao mbali huku ukiweka pamba masikioni kutosikiliza yale wanayoyasema .

📝Maneno ya kukatisha tamaa ni moja ya vyakula vyenye sumu na vilivyochacha ambavyo vitasababisha uone safari yako kuwa chungu .Njiani wakati unaendelea na hatua za ndoto yako utakutana na mambo ambayo unaweza kufikiri kuwa vitakusaidia kukufikisha kwenye hatma ya ndoto zako kumbe vinaua ndoto zako.

📝Achana kabisa na vitu ambavyo havina tija katika safari yako ya kufika pale unapotaka kufika .Sikia siyo lazima kuzingatia kila ushauri unaopewa na watu maana unaweza kukudhuru kama Mla vyote aliyodhurika na chips alizokuwa amenunua akidhani kama zingemsaidia .

📝Iko hivi Mpendwa,utakaporuhusu kila kitu  kuingia masikioni mwako na kwenye ubongo wako kuna wakati ubongo wako utajaa sumu na utaona kila kitu hakiwezekani .

Wakati mwingine nikiwa nafundisha hatua tano za kufikia mafanikio kwenye  Kijana Jithamini niliwaambia kuwa ubongo wa mwanadamu ni kama glasi yenye maji ambayo maji  hayo mtu akiweka sukari maji hayo yatakuwa matamu ,lakini maji hayo hayo mtu akiweka sumu ,ukinywa utakufa```

About Arusha99

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply