Na Sultani Kipingo Mchakato wa uchaguzi mkuu wa klabu Dar es salaam Young Africans Football Club maarufu kama Yanga ulifanyika kwa utulivu na amani na kumalizika salama jana Jumamosi katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salam na matokeo kamili ni kama ifuatavyo: Mwenyekiti Yusuph Manji (pichani juu) alitangazwa mshindi rasmi wa kiti hicho kwa mara ingine tena baada kuzoa kura zote za ndio isipokuwa mbili tu. Yaani alipata kura 1,468 kati ya 1,470 zilizopigwa huku kura mbili tu zikiharibika. Hakukuwa na kura ya hapana. Manji hakuwa na mpizani kwenye nafasi hiyo. Makamu mwenyekiti Clement Sanga ambaye naye pia alikuwa akigombea nafasi hiyo kwa mara ingine kwa kupambana na Titus Osoro, aliibuka mshindi kwa kujizolea kura 1,428 kati ya 1,508 zilizopigwa. Mpinzani wake aliambulia kura 80 tu. Nafasi za 20 za ujumbe ambazo wagombea waliibuka na ushindi katika uchaguzi huo ni: 1. Siza Augustino Lymo (1027) 2. Omary Said Amir (1069) 3. Tobias Lingalangala (889) 4. Salim Mkemi (894) 5. Ayoub Nyenzi (889) 6. Samuel Lucumay (818) 7. Hashim Abdallah (727) 8. Hussein Nyika (770) Idadi ya wajumbe 12 ambao walishindwa kuibuka na ushindi baada ya kura kutotosha ni: 1. David Luhago (582) 2. Godfrey Mheluka (430) 3. Ramadhani Kampira (182) 4. Edgar Chibura (72) 5. Mchafu Chakoma (69) 6. George Manyama (249) 7. Bakari Malima "Jembe Ulaya" (577) 8. Lameck Nyambaya (655) 9. Beda Tindwa (452) 10. Athumani Kihamia (558) 11. Pascal Lizer (178) 12. Silvester Haule (197) http://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js
Tagged with: Sports
About Arusha99
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments