STORY=PIGO MTUNZI_HAIDARI MIRAJI SEHEMU YA KWANZA Asubui na mapema mzee halfani alinyanyuka. Kimya kimya bila ya kumstua mkewe na kwenda kuoga. Aliporudi alipitia chumbani ambapo palikuwa mahususi kwa ajiri ya kulala mtoto lakini badala yake ilipangwa mito na kufunikwa vizuri kabisa. Nilijua tu kama atarudia kufanya vitu hivi tena. Na kila nikimkataza anarudia. Sijui hata nimfanyaje. Alijisemea mzee halfani na kwenda kuitimua ile mito iliyopangwa. Mariamu...! Mariamu...! Aliita mzee halfani baada ya kutoka chumbani na kuingia ndani kwake. We...! Mariamu aliita huku akimtikisa. Bee mume wangu. Aliitaka yule mama aliyelala kwa sauti ya chini. Hivi nilikuambia nini au unataka mpaka siku nikupige ndo unielewe. Aliongea kwa hasira mzee halfani. Ushaanza hivyo haya nimefanya nini tena. Aliuliza mariamu na kusikilizia majibu. Nimeshakwambia sitaki kukuona na midori wala kufunika mito mashuka. Kukosa mtoto ndani ya nyumba kusitufanye tukaonekana hatuna akili. We unafikili wafanyakazi wenzangu wakija. wakikuta umepanga mito watanichukuliaje. Aliongea mzee halfani hadi machozi yakaaonza kumtoka. Naomba unisamehe mume wangu nakuahidi sitorudia tena. Aliongea mariamu. Kila siku huwa unaniambia kama hivyo nakusamehe unarudia. Naona sasa kauli hii imeshakuwa wimbo masikioni mwangu. Ila nimekusamehe na naomba hii iwe ya mwisho. Aliongea mzee halfani na kumbusu mkewe kwenye paji la uso. #itaendelea KWA SASA NITAKUWA NAKIMBIZA HADITHI TATU MJENGONI #MFALME_KATILI #PENZI_UTATA "ii" #PIGO PIGO NI SHORT STORY ITAKAYOKUWA INATEREMKA MJENGONI KILA SIKU UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUSHARE KUCOMENT NA KULIKE #SUPORT YAKO INAITAJIKA
Tagged with: story
About Arusha99
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments