NAHODHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney amepinga kuwa kitendo cha kuchezeshwa kiungo badala ya ushambuliaji kitapoteza ufalme wake kwa taifa hilo. Nahodha huyo alitolewa dakika ya 75 na nafasi yake kuchukuliwa na Jack Wilshere katika mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa na kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Urusi usiku wa jana. Rooney ameviambia vyombo vya Habari vya Urusi kuwa katika maisha lazima mabadiliko yachukue nafasi na yeye anabadilika pia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ndiye mfungaji bora wa Uingereza wa muda wote baada ya kulifungia taifa hilo magoli 50 huku msimu ulioisha akicheza zaidi kama kiungo katika klabu yake ya Manchester United. "Ninajua mpira umebadilika sana siku hizi, mimi kazi yangu ni kufanya kazi niliyotumwa na kocha wangu nitacheza nafasi yoyote nitakayopangwa" alisema Rooney. Rooney alipata majeraha ya goti mwezi Februari ambayo yangesababisha kukosekana katika michuano hiyo lakini alipona mapema na kukiongoza kikosi hicho cha 'Watoto wa Malkia' Three Lions. Akizungumzia sare waliyoipata katika mchezo wao wa awali nahodha huyo alisema bado wanayo nafasi ya kufanya vizuri kwakuwa wana wachezaji vijana wenye vipaji ambao watalibeba Taifa hilo. http://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js
Home
»
»Unlabelled
» NAHODHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney amepinga kuwa kitendo cha kuchezeshwa kiungo badala ya ushambuliaji kitapoteza ufalme wake kwa taifa hilo.
Tagged with:
About Arusha99
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments