Select Menu

Slider

Powered by Blogger.

Music

Health

Sports

News

Photos

Documentary

Video

» »Unlabelled » LIONEL MESSI ACHEKELEA KUREJEA UWANJANI NA 'HAT-TRICK' LIONEL MESSI ACHEKELEA KUREJEA UWANJANI NA 'HAT-TRICK' A+A- PrintEmail Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/06/lionel-messi-achekelea-kurejea-uwanjani
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

 STRAIKA Lionel Messi amesema anajisikia mwenye furaha baada ya kuingia uwanjani kipindi cha pili na kutupia ‘hat-trick’ na huku nahodha huyo wa Argentina akiwapongeza wachezaji wenzake kwa kuweza kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Copa America Centenario. Baada ya wiki iliyopita kuwekwa benchi katika mechi ya kwanza ambayo waliibuka na ushindi dhidi ya mabingwa watetezi kutokana na matatizo yake ya mgongo, juzi Messi alirejea uwanjani akiwa na pumzi mpya baada ya kufunga mabao matatu ndani ya dakika 30 yaliyoifanya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Panama ambayo ilimaliza mchezo huo uliopigwa mjini Chicago ikiwa na wachezaji 10. Nahodha huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye ‘hat-trick’ ilikamilika dakika ya 78 kwa mpira wa adhabu, kwa sasa amefikisha bao lake la 53 katika timu ya taifa na huku akiwa anapungukiwa matatu ili kuwa mfungaji bora wa muda wote katika kikosi hicho cha Argentina. Akizungumza baada ya mtanange huo wa kundi D uliopigwa kwenye dimba la soldier Field, mchezaji bora huyo wa mechi alisema kwamba anajipongeza kwa msaada huo wote. “Ni jambo kubwa kuwa mahali hapa, hususan kwa sababu ya kadamnasi. Najivunia sana,” alisema staa huyo. “Nimepoteza maumivu na kisha nikafanikiwa kufunga bao langu la kwanza.” “Hizi ni jitihada za timu, ilikuwa ni mechi ngumu iliyochezwa kwenye nyasi ndefu na kavu, ilikuwa ni mbinu lakini tumefanikiwa kufikia tulipopataka,” aliongeza staa huyo wa Barcelona. http://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js

About Arusha99

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply