Select Menu

Slider

Powered by Blogger.

Music

Health

Sports

News

Photos

Documentary

Video

» » KILIMO CHA Zana bora za kilimo kikwazo kilimo cha ufuta Chalinze POSTED ON JUNE 09 2016
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

KUKOSEKANA kwa wataalam wa ugani na zana bora za kilimo imekuwa ni changamoto kubwa inayomkabili mkulima wa ufuta jimbo la Chalinze mkoani Pwani. Ufuta ni zao la biashara ambalo limeanza kulimwa kwa wingi katika mkoa wa Pwani,hasa jimbo la Chalinze kutokana na soko lake kuongezeka kila msimu. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara,mbegu za zao hili huwa na wastani wa mafuta kiasi cha asilimia 45, hata hivyo wakulima wake wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa nyenzo na elimu. zao hilo limeanza kulimwa kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni katika eneo hilo baada ya soko lake kuongezeka kutoka sh.1000 kwa kilo miaka mitatu iliyopita hadi sh.2800 kwa kilo. Hata hivyo licha ya wakulima wengi waliokuwa wamekata tamaa na kilimo cha mahindi kuamua kuingia sasa shambani kulima ufuta wameanza kukabiliana na changamoto nyingine. Katika baadhi ya maeneo hususani kata ya Lugoba watalaamu wapo lakini wanadai kuwa hawana usafiri wa kufika kwenye maeneo ya wakulima kila mara ili waweze kutoa elimu inayotakiwa kwa wakati muafaka. Awali wakulima wengi walikuwa wamesusa kilimo cha mahindi kutokana na kukosekana kwa mvua za kutosha, zana za kilimo na mazao kuharibiwa na mifugo. Hali iliyochangia ugumu wa maisha katika jimbo hilo na njaa za mara kwa mara lakini sasa baada ya wakulima kugeukia kilimo cha ufuta ambacho wanaamini kuwa mazao yake hayasumbiliwi na wanyama kama ng’ombe maisha yameanza kubadilika. Kutokana na kukosekana kwa zana bora za kilimo kama matrekta au jembe la ng’ombe wakulima wamekuwa wakitumia mkono hivyo kuambulia kulima eneo kidogo nakushindwa kujikomboa. Felex Butahe ni mkulima ambaye ameanza kulima zao hilo katika kijiji cha Lugoba Kata ya Lugoba,amefanikiwa kulima heka 5 lakini kwa kuwa hakuwa na elimu ya kilimo hicho wala hakuweza kumpata mtaalam amelazimika kutumia kilo 10 za ufuta badala ya kilo moja. “kwa kweli gharama ya kilimo hapa chalinze ipo juu ni vigumu kwa mtu wa kawaida kuimudu kwani nimelima kila heka nilitumia shilingi 70,000 kwa trekta na ufuta nikatumia sh.40,000 sawa na sh.4000 kila kilo”anasema kwa masikitiko. Felex anasema ilipofika kipindi cha kupalilia amelazimika kutenga shilingi 45,000 kila heka jambo ambalo limegarimu hela nyingi, ikilinganishwa na mkulima wa mahindi kule Dodoma ambaye anataumia shilingi 20,000 kulima heka ya mahindi. Hata hivyo felex anasema kuwa tangu aanze kulima eneo hilo hajawahi kukutana na bwana kilimo ampe ushauri namna ya kulima ufuta kwa njia bora ili aweze kunufaika. Malalamiko hayo yanaungwa na mkono na mkulima mwingine anayefahamika kwa jina la Mchungaji William yeye anasema kuwa ameishi eneo hilo siku nyingi lakini hajawahi kuwaona maafisa kilimo wakiingia mashambani kuwafundisha namna ya kulima kilimo chenye manufaa. “Hapa kwetu kumuona Afisa kilimo labda shamba limeliwa na wanyama sasa anakuja kuangalia ili atoe taarifa lakini sio kuja kutusimamia namna ya kulima hata shamba darasa hilo hawafanyi”anasema Mchungaji Wiliam. Kauli hiyo imepingwa na afisa Kilimo wa kata hiyo John Tualigo ambaye amesema kuwa wamekuwa wakifanya kazi yao lakini tatizo kubwa ni usafiri wa kutumia kuwafikia wakulima hao. “Sio kweli, tunakwenda mashambani kama mimi, nimesimamia kikundi cha wakulima katika kijiji cha Saleni tumeweza kupokea mbegu nzuri kutoka shirika la MUVI ,wakulima wamelima msimu uliopita wakavuna zaidi ya Kilo 600 za ufuta ambazo wameuza kwa shilingi 2800 kila kilo na sasa wamezitumia kulima heka 42”anasema Tualigo Anasema kuwa changamoto inayowakabili wasiwafikie wakulima kiurahisi ni usafiri kwani hata yeye alikuwa na pikipiki kama afisa Kilimo wa kata lakini ina miezi mitatu haifanyi kazi licha ya kutaalifu mwajiri wake. Tualigo anasema kuwa wakulima wa Saleni walipokea mbegu aina ya Lindi II ambazo hutoa mavuno mengi baada ya kufanyiwa utafiti na kituo cha utafiti Naliendele Mtwara. Anasema kuwa awali kikundi hicho kilikuwa na wanachama 13 lakini sasa wamefikia 32 katika msimu huu wanatarajia kuvuna zaidi ufuta ili mbegu ziuzwe katika vijiji vingine ambavyo havijapata mbegu hiyo. “Mwaka jana walikuwa wakulima 13 wakalima heka 9 wakavuna tani 2 katika msimu huu wamefanikiwa kulima heka 48 baada ya wanachama wengi kuongezeka hasa baada ya wakulimakuvutiwa na mafanikio waliyopata wale wanakindundi ambao walililipia watoto ada shuleni na wengine wakajenga”anasema Tualigo Anasema kuwa lengo la mradi huo ni kwenda kwenye vijiji vyote sita vya kata hiyo lakini njia rahisi ya kuafikia wakulima hao inashindikana baada ya kukoseka kwa nyenzo mbali mbali ikiwemo usafiri, hali inayofanaya wakulima wengi kupanda ufuta bila utaalm kwa kutupa tupa mashambani na kutumia mbegu nyingi. Naye afisa kilimo wa kijiji cha Saleni,Rashid Ali,akizumgumza katika mashamba ya ufuta yaliyolimwa na kikundi cha Saleni Seasame Farm Group, amewashauri wakulima kuungana kama walivyofanya wakulima wa kijiji hicho ambao wamefaidika kuuza ufuta kwa pamoja katika msimu uliopita,ambapo Kilo moja iliuzwa kwa sh.3000 badala ya 2000 iliyouzwa mitaani. Amewashauri wakulima kupanda mbeguza ufuta nusu inchi, chini ya udongo, inchi sita umbali wa mbegu na mbegu na futi mbili nafasi ya msitari na msitari, kabla ya kupanda wahakikishe ardhi imelainika vya kutosha na upande mbegu masaa mawili au matatu baadae. Afisa kilimo huyo amesemakuwa mbegu za Lindi 2002 zikilimwa katika eneo lililoandaliwa vizuri na kupaliliwa mapema ,mkulima anaweza kuvuna kilo 500 hadi 600 kwa heka tafauti na mbegu za kienyeji ambao mkulima huambulia kilo 100 hadi 200 kwa heka. Hata hivyo maafisa hao wanasema kuwa wakulima wakiungana na kulima zao kwa pamoja inakuwa rahisi kuhudumiwa na wataalam, wakati wakutafuta soko ni rahisi kupanga bei na takwimu za mavuno hupatikana kirahisi,hata kijiji hufaidika na ushuru wa soko. Mbegu mpya za lindi zimetajwanawakulimawengi waliozitumia msimu uliopita kwambazimeonyesha kuwavutia kutokana na ukweli kwmaba ni nyeupe na kubwa ikilinganishwa na hizi zingine za kawaida. Jasintha Wiston mkulima wa Tonga kata ya Msoga anasema “ nimeanza kutumia mbegu mpya inaitwa LINDI 2002 Eka 1 unapata gunia 8 hadi 12 tafauti na zilembegu za kienyeji ambazo huambulia kiduchu”. Wiston anasema mpaka kufikia mavuno anatarajia kuvuna kilo 300 za ufuta kwa kila heka moja na kwamba bei ya ufuta kwa kilo ni zaidi ya shilingi 2800 hivyo msimu huu anaweza kupata bei zaidi. “Katika fedha za mkopo nilizopata zilinisaidia kung’oa visiki na kulima kwa kutumia trekta la kukodisha na ndio maana nina matumaini ya kupata mavuno mengi katika msimu huu kwa sababu nimetumia kilimo cha kisasa zaidi: Kama ingekuwa ni jembe la mkono nisingeweza,” anasema mkulima huyo. Hata hivyo anaiomba serikali na wafadhili mbalimbali kutambua kuwa kilimo pekee ambacho kitamkomboa mkulima ili kuondokana na umaskini ni kilimo cha kutumia zana za kisasa na kwamba hata powertiller zinazotolewa bado hazina tija kwa mkulima kutokana na kushindwa kulima meneo yao. Mkulima mwingine anasema msimu uliopita amevuna magunia 10 ya ufuta baada ya kutumia mbegu za Naliendele, Ziada na Lindi White alizopatiwa na muungano wa vikundi vijijini muvi na kuuza gunia moja kwa Sh 240,000 na kupata Sh2.4 milioni. Mkulima huyo anatoa ombi kwa Serikali kuanzisha bodi ya zao la ufuta kama ilivyoanzisha bodi ya mazao ya pamba, kahawa na katani ili kuwainua wakulima kiuchumi wa zao la ufuta. Mafuta ya ufuta hutumika katika mapishi mbalimbali ili kuongeza ladha. Pia husaidia kuleta nguvu na joto mwilini. Mbegu za ufuta huchanganywa na vyakula mbali mbali kama mikate, keki, mboga na kadhalika. MAMBO YA KUZINGATIA WA KATI WA KUZALISHA MBEGU • Chagua aina ya mbegu inayotoa mazao mengi na bora, inayovumilia mashambulizi ya magonjwa na wadudu, inayokomaa mapema na kutoa mafuta mengi. unaweza kuchagua mbegu inayokomaa kwa pamoja ili kurahisisha uvunaji na pia kuepuka upotevu wa zao shambani. aina nyeupe ya mbegu ya ufuta hupendelewa zaidi kuliko aina nyeusi. ufuta nahitaji rutuba ya kutosha ili kutoa mazao bora. Katika kudumisha rutuba ya udongo, tumia kilimo cha mzunguko wa mazao au weka mbolea za asili pale inapobidi. kitaalamu inashauliwa kuwa mkulima adhibiti magugu kwa kupalilia ili kuruhusu ufuta kutumia vizuri unyevu na virutubishi. Magugu mengine huwa ni maficho ya wadudu waharibifu wa zao la ufuta. MAGONJWA NA WADUDU Ufuta hushambuliwa na magonjwa na wadudu mbalimbali ambao huweza kusababisha upungufu na ubora wa mazao. Hivyo kagua shamba mara kwa mara hasa kwenye maua na mapodo ili kuona dalili za mashambulizi. Endapo kuna dalili zama shambulizi, chukua tahadhari mapema kabla ya uharibifu mkubwa haujatokea. unaweza pia kukagua shamba kuona kama ufuta umekomaa. , Ufuta hukomaa, kati ya miezi mitatu na minne tangu kupanda kutegemea aina ya ufuta usiokuwa na matawi hukomaa mapema kuliko ile yenye matawi ni muhimu kuwahi kuvuna ili kuepuka ufuta kupukutikia shambani. KUKAUSHA Mapodo ya ufuta hukaushwa yakiwa yamefungwa katika vitita. Vitita huwekwa kwa kuegeshwa kwenye fremu ya kukaushia kwa muda wa wiki mbili hadi tatu kutegemea hali ya hewa. Fremu hii huwekwa juu ya turubai au sakafu ili kuzuia upotevu wa punje kutokana na kupasuka kwa mapodo.

About Arusha99

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply