INAWEZEKANAJE MTU KUPATA MILIONI 890 NDANI YA MIAKA MITANO?(1) Unapotaja milioni 890, kila mmoja ataitazama kwa namna yake. Kwa mwingine ni pesa nyingi kupindukia, kwa mwingine ni pesa ya kawaida lakini kwa mwingine ni
http://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js
pesa ndogo sana. Nafahamu kwamba mazoea, mazingira na uzoefu ndivyo vinapelekea watu kufikiri kwamba milioni 890 ni kiwango kikubwa mno. Kwa mtu anaelipwa mshahara wa milioni moja(1,000,000/=) kila mwezi, itamchukua miaka takribani sabini na nne(74) kupata milioni 890 kupitia mshahara! Yaani Tsh. 1M*12(miezi ya mwaka mmoja) *74(miaka)= Tsh. 890M. Kwa mfanyakazi anaelipwa shilingi laki tano itamchukua miaka mia moja na arobaini na nane ili kupata milioni 890! Yaani 0.5M*12*148=Tsh. 890! Hata mtu anaelipwa mshahara wa milioni tano kwa mwezi itamchukua miaka 15 kufikisha milioni 890. Yaani Tsh. 5M*12*15= Tsh. 890M Pia nafahamu kwamba unapotaja mshahara wa milioni moja kwa mwezi, ndio mishahara ya watu ambao kwa wastani wanaonekana kuwa na kazi nzuri! Unapotaja watu wanaolipwa milioni tano kwa mwezi, hao wanahesabika kuwa kama wateule na kimsingi katika nchi kama Tanzania wapo wachache sana. Mishahara mingi ya wafanyakazi inacheza chini ya milioni mbili. Vile vile nafahamu kuwa viinua mgongo vya wafanyakazi wengi huwa havizidi milioni mia moja(100,000,000/=) Ikiwa hata wanaolipwa milioni tano kwa mwezi bado hawawezi kuzichanga milioni 890 ndani ya miaka mitano:- inakuwaje hawa BU waje na dhana ya mtu kupata milioni 890 ndani ya miaka mitano? Wanautoa wapi ujasiri huu? Cha kustaajabisha ni kwamba inasemwa kwamba hili linawezekana kwa mtu yeyote iwe ana kipato ama hana, iwe ana mshahara mdogo ama mkubwa! Haya ni maswali na mshangao ambao watu wengi wanaposikia milioni 890 kwa miaka mitano wamekuwa wakituuliza na kushangaa! Wengine huwa hawajichoshi hata kuuliza bali huishia kusema, "Haiwezekani"! Kabla sijakupigia hesabu za mambo kadhaa unayoweza kufanya na kukamata milioni 890 ndani ya miaka mitano:- nataka nikuoneshe namna milioni 890 inavyofanana. Je, Tsh. Milioni 890 ni kiwango kikubwa sana? Hivi unadhani kiwango hiki cha milioni 890 ni kubwa basi? Wala hataaaa! Hiki ni kiwango kinachokamatika kwa urahisi kabisa. Unajua nini? Ukitaka kujua kwamba hiki kiwango si chochote wala si lolote tazama milioni mia nane tisini inafananaje:- Ukichukua milioni 890 ukaenda kununua malori yale ya Howo (roli na tela lake) ama ukanunua Scania Used(na tela zake) utapata malori sita tu (kwa makadirio ya bei ya Tsh Milioni 120-150 kila moja). Sasa hebu niambie, wewe ukiwa na Malori sita mjini kwani ni utajiri wa kusema utatikisa mji? Walaa hata! Si unaona milioni 890 zilivyo za kawaida enhee? Sasa, achana na malori maana huenda unayagwaya sana "masemi-trela":- Chukua milioni 890 nenda kajenge nyumba za maana (kiasi flani) maeneo ya Njiro pale Arusha, ama maeneo ya Mbezi pale Dar es Salaam ama maeneo ya Kapri Pointi pale Mwanza ama maeneo ya ForestMpya pale Mbeya ama maeneo ya Gangilonga kule Iringa. Hizo hela kama ukianzia kununua viwanja na kujenga katika maeneo hayo huwezi kukamilisha majengo ya maana zaidi ya “mawili”. Tena kama pale Njiro Arusha hata "mjengo" mmoja unaweza usiishe, maana kiwanja peke yake utasikia milioni mia mbili! Sasa tufanye kote huko umefanikiwa kupata "mijengo yako miwili", paaapu, umetulia! Nikuulize swali:- hivi kumiliki nyumba mbili(ama iite mijengo miwili) ni kitu kinachoweza kukufanya utikise mjini? Ahaa, sitaki kukulinganisha, lakini ujue watu wana nyumba hadi ishirini na bado hela(ama thamani yao) sio ya kutisha, yaani, vijana tunasema, kawaida sana! Mwingine bado ataniambia, “Ohoo, Spika, unajua milioni 890 ni hela nyingi sana” Usipate taabu, ngoja nikuoneshe milioni 890 inavyofanana kwa upande mwingine. Unajua ukichukua milioni 890 ukaenda kununua magari aina ya LandCruiser V8, Unapata magari mawili pekee na chenji inayorudi inaweza isitoshe hata kununua kiwanja cha ekari moja pale Bunju Dar es Salaam? Hivi mtu akiwa na magari mawili (tu V8 tuwili) utasema ni utajri wa kuutetemekea? Kwanza magari mawili yanatosha wewe na mume wako hata watoto wanakuwa bado hawajapata usafiri! Kuwa siriazi bana, acha masikhara na maisha, atiii! Milioni 890 ni kitu gani hadi kinakufanya unapoisikia unakuwa mdogo kama piritoni, usiniangushe bana! Usitishike na milioni 890 kwa sababu ikianza kujenga hospitali ndogo tu ya kawaida inaweza ikaishia njiani hata isifanikiwe kumalizia chumba cha mochwari! Nikwambie kitu? Tunaposema milioni 890 ujue ni “hela za kawaida sana" na wala usitishike wala kuogopa. Achana na wale ambao hawajaelewa wala kusikia "udogo wa milioni 890 kwa yale inayoweza kuyafanya":- , wewe tulia hapa, uone tunavyosaidiana maarifa na msaada wa kuicheza hii ngoma ya "umilionea". Unajua ni nini tena? Ndio maana tumesema kwamba milioni 890 ni kianzio, ama twasema kima cha chini kabisa. Tafsiri yake ni kwamba mbingu ndio ukomo wako, waweza kamata bilioni, bilioni kumi n.k Ni wewe tu, lakini hii kiwango nakuthibitishia kinawezekana tena kiurahisi sana kuliko ulivyodhani! Acha kuwafuatilia hao wa “jero-jero”, kaa hapa na sisi wenzio tunaowaza “kimilioni-milioni” Ngoja niliseme na hili pia:- Hivi unajua kwamba ukiwa na shilingi elfu moja ni rahisi sana kuikamata elfu kumi? Najua unajua! Hivi unafahamu kwamba ukiwa na elfu kumi inakuwa simpo kuiwazia laki moja, tofauti na mtu mwenye elfu moja kuiwazia laki moja? Hata kama ulikuwa hufahamu ndio nishakufahamisha hivyo. Na unajua kuwa kama laki zinapita-pita mikononi inakuwa fasta kukamata milioni, si ndio enhee? Basi sasa ni rahisi kujua kwamba milioni mia moja inafikika kirahisi kwa kuanza na milioni kumi iliyotoka kwenye milioni moja, iliyozalishwa kutoka laki moja, mdogo wake wa elfu kumi na mjukuu wa elfu moja! Unajua ninachotaka kukueleza? Ni hiki:- maadamu umepata fursa ya kuonja mafundisho na mikakati ya BU ili kuisaka milioni 890, upo sahihi sana bila kujali utaanza na kiasi gani! Chochote ulichonacho kinatosha kuanza nacho na hatimaye kufikia ndoto ya milioni 890 ndani ya miaka mitano. Usikonde wala kuogopa hata kidogo, maana tutakupa njia za kupita! Unajua ni nini tena? Iko hivi, kadiri unavyopanda juu kifedha(ama kadiri fedha zinavyoongezeka) ndivyo mwendokasi(spidi) wa hela kukujia unavyoongezeka. Andika kwenye daftari hii pointi:- muda utakaotumia kupata elfu kumi kutokana na elfu moja uliyoanza nayo utakuwa ni mkubwa kuliko muda utakaotumia kupata laki moja kutoka kwenye elfu kumi utakayoizalisha. Nakuongezea pointi hii:- muda utakaotumia kupata milioni 100 kutoka kwenye milioni kumi uliyofikia utakuwa ni mfupi zaidi ukilinganisha na muda ulioutumia kuzalisha milioni kumi kutoka kwenye milioni moja. Si umeshajua kitakachotokea kuhusu milioni 890 utakaposhika milioni mia moja, enhee!? Maana yake ni nini? Ni kwamba unaweza kuifikia milioni 890 ndani ya muda mfupi sana kutegemea unatumiache kile ulichonacho sasa hata kama ni kidogo namna gani. Kazi yetu ni kukuonesha thamani na namna ya kutumia ulichonacho ili ufike nchi ya milioni 890 tunayokueleza habari zake. Sehemu ya pili nitakuja kukuonesha ulimwengu wa milioni 890, na kukupa mahesabu kadhaa ya fursa yanayokuonesha namna kadha wa kadha za kufikia uhuru wa kiuchumi ama uite umilionea wa kiwango cha milioni 890
No comments