HOFU NI BANDA BOVU!!!!! Sababu kubwa ya watu wengi ikiwa ni pamoja na wewe kutotimiza malengo yako ni HOFU
http://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js
. HOFU ni kitu kimoja kibaya sana katika safari ya mafanikio yako. Kila mmoja anatamani na anatafuta mafanikio ila tatizo mioyo yetu imejaa HOFU. Hofu ndio kikwazo cha mafanikio na maendeleo yetu ktk maisha.Kila mtu ana hofu msomi mwenye elimu na ujuzi ana Hofu na asiye na elimu naye pia ana Hofu tena Mara mbili ya mwenye elimu na maarifa. Tajiri nae ana Hofu juu ya usalama wake na Mali zake. Maskini ndio usiseme ana hofu zaidi maana hata kesho yake haijui itakuwaje na itafikaje. Kifupi ni kuwa kila mtu kwa namna yeyote ile ana Hofu. Kisaikolojia kuna aina kuu mbili za Hofu bila kujali ni kundi gani la watu maskini au tajiri.Hofu ya kwanza ni HOFU YA KUSHINDA na HOFU ya Pili ni HOFU YA KUSHINDWA. Hizi ndizo Hofu kuu mbili zinazotuzuia sisi binadamu kutimiza malengo yetu ktk kufikia na kutimiza ndoto zetu ktk maisha.Haijalishi ni Hofu gani unayo ila una Hofu hapo ulipo hata ukinikatalia Mim ila ukijichunguza utakubaliana nami kuwa una Hofu. By the way siku kutaka kujua una Hofu ya nini lengo langu ni kukuelimisha kuwa Hofu ndio kikwazo ktk kupata kile unataka ktk kutimiza ndoto zako za Mafanikio. Hofu ya kushindwa ndio mbaya zaidi kuliko Hofu ya kushinda kwani Hofu ya kushindwa kuua moyo na kukatisha tamaa ya kutojaribu hata kufanya jambo. Ila Hofu ya kushinda inaweza kumpa moyo wa kufanya jambo japo si kwa kiwango kikubwa cha kufikia mafanikio ayatakayo.Zipo njia mbalimbali kama 30 za kukabiliana na Hofu hapa ktk makala yangu naomba nikupe 3 tu zingine tutaendelea kupeana ktk makala zijazo. Mbinu au siri za kukabiliana na Hofu hizi mbili. 1.Jiamini - ktk maisha yako unapaswa kujiamini na kuwa mwaminifu ktk kauli na vitendo vyako. Utaepukana na uwongo na udanganyifu utakao kusababishia uishi kwa Hofu ya kugundulika uwongo wako. 2.Tafuta Maarifa- Soma na uwe na elimu nzuri itakayoweza kukuongoza ktk kufanya mambo kwa usahihi na kwa ueledi MKUBWA.kukosa maarifa na elimu ni mwanzo wa kuwa na Hofu kwa sababu utafanya vitu ambavyo huna uhakika navyo. 3.Kuwa mdadisi-Kamwe ktk maisha yako usiamini kila unachoambiwa na kukiamini 100% kuwa ni kweli na ndivyo ilivyo jitahidi kutafakari na kuchunguza kwanza je ni kweli inawezekana? Kwa nini iwe hivyo? Usimuamini kila mtu Mara nyingi HABARI yeyote ya kuambiwa INA uwongo 99% kwa sababu msemaji ni lazima atatia chumvi kwa maana ya kupunguza au kuongeza baadhi ya Maneno yasiyokuwepo. Ndipo pale Mimi Frank Luoga huwa napenda kusema AKILI YA KUAMBIWA CHANGANYA NA YAKO KUPATA UKWELI WAKE. Mafanikio yanahitaji Moyo usiyo na Hofu/mashaka na wasiwasi. Vitabu vitakatifu vinatuasa kuwa "JAMBO LOLOTE UKIWA NA HOFU, MASHAKA AU WASIWASI NALO USILIFANYE KWA MAANA HUTALIFANYA KIKAMILIFU" Hii ni kutuonyesha namna gani Hofu ni mbaya na inaathari ktk kufanikisha mambo yetu katika maisha.Kuna kauli huwa napenda kuwaambia na kuwashauri wachumba wanaotaraji kuoana kuwa kamwe usikubali kuolewa au kuoa mtu ambaye bado una mashaka nae ndoa yenu itakuwa na mashaka mashaka kamwe hamtoaminiana ndani ya ndoa yenu. Kila siku hakutisha migogoro na visa. Vivyo hivyo ktk mafanikio ukifanya jambo lililo na mashaka nalo lazima lifeli.Kila mtu anayo haki na wajibu ktk kupambana na Hofu ili afanikiwe ktk maisha yake. CHUKUA HATUA LEO IDHIBITI HOFU UPATE NJIA SAHIHI YA KUFIKIA MAFANIKIO YAKO NA KUTIMIZA NDOTO ZAKO.
No comments