Select Menu

Slider

Powered by Blogger.

Music

Health

Sports

News

Photos

Documentary

Video

» » Twitter kufanyiwa mabadiliko ili kuwavutia watumiaji
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Mtandao wa Twitter unafanyia marekebisho sheria zake ili kuwarahasishia kazi watumiaji wake na kuufanya uwe wa kuvutia kwa wale wanaojiunga nao kwa mara ya kwanza. Wanachama wa mtandao hao sasa wataweza kuongeza kile wanachochapisha kwenye mtandao huo, zikiwemo picha na video bila ya kuathiri kiwango cha sasa cha maneno 140 ambayo mtu anastahili kuandika. Twitter pia itafanya marekebisho kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana katika mtandao. Image copyrightPA Image caption Twitter imekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia. Mwanzilishi mwenza wa Twitter na mkurugenzi mkuu Jack Dorsey, aliiambia BBC kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa wakati watu wanapoutumia unaonekana kuwa ulio na maana. Mdadisi mmoja anasema kuwa hatua hizo zinaashiria mwelekeo mwema, lakini akaongeza kuwa wameangazia suala moja tu ambalo ni kuongeza watumiaji wake. Licha ya mtandao huo kutumiwa sana katika masuala yanayohusu habari mwaka uliopita, umekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia. Image copyrightREUTERS Image caption Twitter pia itafanya marekebisho kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana katika mtandao. Brian Blau, ambaye ni mchambuzi kutoka shirika la Gartner, anasema matatizo yanaoikumba Twitter kuwapata watumiaji wapya hayawezi kutatuliwa na mabadiliko hayo. Anasema kuwa tatizo kuu ni kuwavutia watumiaji wapya na kuwafanya wawe wazalendo kwa mtandao. A

About Arusha99

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply