Na Mwandishi wetu. Leo katika makala za kajamii tujifunze nakuzitambua faida za Tango katika miili yetu, ikiwa watu wengi tunakula bila kujua faida zake katika maisha ya kila siku. Watu wengi tunapenda matunda Fulani kwa ladha yake tuu bila kutaka kupata faida, katika mwili ikiwa faida ya baadhi ya matunda ni pamoja na radha yamatunda mabalimbali.  1. Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B. 2. Tango huupa mwili na vitamin. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku. 3. Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa machoni na kuondoa vimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani tango lina virutubisho vya kuondoa vimbe hizi na pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele. 4. Tango lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume. 5. Tango husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani. 6. Tango huondoa hangover kwa watumiaji wa pombe kwani lina vitamin B ambazo husaidia kupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.  7. Tango husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri. Kutokana na kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kiasi cha maji kilichopo kwenye tango na Kamba Kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula. Unapokula tango kila siku pia hukusaidia wewe mwenye choo kigumu au usiyepata choo kabisa kwa muda mrefu kuondokana na tatizo hilo. 8. Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood pressure). Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari. Pia watafiti wamegundua kuwa kuna kirutubisho kiitwacho sterol kwenye tango ambacho husaidia kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu. Tango lina kiwango kikubwa cha potassium, magnesium na Kamba Kamba ambazo husaidia sana kudhibiti shinikizo la damu aina zote yani high blood pressure na low blood pressure. 9. Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis). Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo (connective tissue). Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid). 10. Kutokana na maji na virutubisho vilivyopo kwenye tango, tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda. Nadhani tutakuwa tumeelimika kwa kufahamu umhimu wa tunda aina ya tango ikiwa tunda hili halivutii kula kwa kuwa halina radha nzuri sana pia halina harufu inayosikia kuwa hili ni Tango kwa kukazia tango lina asilimia kubwa ya maji. Zingatia Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida. Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha potassium kama tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye tatizo la moyo, shinikizo la chini la damu.
Tagged with: Health
About Arusha99
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments