AMKA NA MBINU ZA KUONGEZA MAUZO YA BIASHARA YAKO. Mzunguko wa fedha ndio damu ya biashara yako. Kama mzunguko huu wa pesa haupo vizuri basi biashara yako itaadhirika na kama mzunguko huu utasimama basi biashara yako itakufa kabisa. Leo tunaangalia eneo muhimu sana la kuhakikisha mzunguko wa fedha kwenye biashara yako unakuwa mzuri. Eneo ili ni mauzo. Mauzo ndio huleta fedha kwenye biashara yako na hivyo kama ukiongeza MAUZO maana yake unaongeza fedha. Japokuwa hii haimanishi kwamba ukiongeza mauzo basi ndo umeongeza faida. Leo tuangalie kwanza kuhusu mauzo ya biashara yako na namna gani ya kuyaongeza. Kabla hatujaona mbinu tano ambazo unaweza kuzitumia kuongeza mauzo kwenye biashara yako naomba nijibu swali muhimu sana ambalo wewe unaweza kujiuliza. Je inawezekana mauzo ya biashara yako kuongezeka....?? Jibu ni NDIO, haijalishi biashara yako ipo kwenye hatua gani, bado una nafasi ya kuongeza mauzo zaidi ya unayoyafanya sasa kikubwa ni wewe kujua mbinu sahihi za kutumia ili uweze kuongeza mauzo yako. Mauzo ya biashara yako yanaweza kuongezeka, sasa unayaongezaje....?? Hapa ndio zinakuja mbinu tano muhimu zinazoweza kutumiwa kuongeza mauzo yako. MBINU YA KWANZA; Uza bidhaa zinazoendana kwa pamoja. Mteja anapokuja kununua bidhaa kwako, tayari amejipanga atanunua bidhaa au huduma fulani. Unaweza kumuuzia bidhaa hiyo na akaondoka unakuwa umepata mauzo ya kile alichokitaka na mambo yanaishia hapo. Ila ukiwa mfanyabiashara mjanja unaweza kumuuzia bidhaa anayotaka na pia ukamjulisha kwamba kuna bidhaa nyingine ambayo inaweza kuwa na matumizi sawa na kile alichochukua. Au endapo bidhaa hizo zitatumika kwa pamoja basi zinaweza kuboresha maisha yake kwa kiasi kikubwa. kwa mfano; kama mtu amenunua nguo, muuzie na viatu na begi la nguo. Kama amenunua kompyuta mwambie kuna vitu muhimu anahitaji kununua ambavyo vitafanya matumizi ya kompyuta yake kuwa mazuri. Kwa mfano kuweza kuhifadhi data zake sehemu tofauti ili zisipotee kompyuta inapopotea. Kama mtu akinunua kitabu kimoja muoneshe na vitabu vingine ambavyo vitampatia maarifa zaidi. Kwemye biashara yoyote unayofanya kuna bidhaa nyingi unazoweza kuuza kwa pamoja. Fanyia kazi hili. MBINU YA PILI; Uza bidhaa yenye uhitaji mkubwa. Ni rahisi kwa mtu kununua tiba kuliko kinga. Ndivyo binadamu tulivyo, kama hakuna tatizo juu ya kitu fulani basi hatuangaiki kupata suluhisho. Ni kazi yako wewe kama mfanyabiashara kuangalia biashara ina matatizo gani ambayo yanaumiza vichwa vya watu na wanatafuta suluhisho lake. Kisha wapatie suluhisho la matatizo yao kupitia biashara yako. Siku njema ya mafanikio
Tagged with: business
About Arusha99
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments