Angalia jinsi maisha yanavyozidi kuwa magumu katika jamii zetu. Gharama za vyakula, usafiri, na mambo mengine zinazidi kuongezeka, pia mabadiliko ya kiteknolojia na kijamii yanaleta changamoto nyingi. Tupo katika zama ambapo kusimama kiuchumi kunahitaji kujidhatiti kweli kweli. Makala hii inachambua mambo ya msingi ambayo yanaweza kukusaidia kujipanga kupata dili zinazoweza kuinua maisha yako.
1. Jitafakari:
Ni vizuri kujizoesha kutafakari kuhusu wewe ni nani, mapungufu yako, mambo gani makubwa na mazuri uliyokwisha wahi kufanya, na vitu gani hasa unavipenda na usivyovipenda. Tafakari hii itakupa picha ya aina gani ya mtu wewe ulivyo, na kukusaidia kujipanga kuziba yale mapungufu, na wakati huo huo, utaweza kuangaza fursa zilizopo na unazoweza kuzitumia kutokana na 'ubora' ulionao.
Tafakari hii itakuwezesha pia kutambua kitu kiitwacho kwa kiingereza 'passion', yani mambo unayoyapendelea sana kufanya au kuwa hapo baadae. Umuhimu wa kutambua passion ni kwamba ukiweza kuwekeza muda katika passion yako inaweza kuwa sehemu nzuri ya kujijengea maisha yenye furaha. Kwani passion itakufanya ufanye jambo utalotaka kulifanya kwa ufanisi na pia hata ukikumbana na changamoto, hautokata tamaa kirahisi rahisi.
2. Mambo mazuri hayataki haraka
Kumbuka hao wote unaowaona wamefanikiwa kimaisha, mafanikio ambayo pengine unatamani uwe nayo, sio kwamba mafanikio hayo yalikuja kwa siku moja. Kuna maandalizi kadhaa waliyafanya, magumu waliyoyapitia mpaka kufika hapo walipofika.
Hii kwako ina maana kuwa ni lazima ujue kuna muda ni lazima uutumie kufanya maandalizi, inabidi utambue kuwa utakutana na magumu, ila hautakiwi kukata tamaa. Na zaidi sana ni lazima ujue bidii inahitajika. Hata hivyo bidii zako zitazaa matunda kwa haraka kama utatambua mapungufu yako mapema, na pia passion yako hasa ni ipi. Ukitambua mapungufu yako mfano una tatizo la lugha ya kiingereza, basi utafanyia kazi pungufu hilo ili uwe bora zaidi.
3.Utafiti ni muhimu sana
Ni muhimu sana kuwa na taarifa sahihi kuhusu nini vinaweza kufanikisha mipango yako na matarajio yako ya kimaisha. Mfano kama unatamani kufanya biashara, basi tafakari aina gani ya biashara, tafuta taarifa za kutosha kuhusu wateja wa biashara husika, kiasi cha mtaji , mbinu za kimasoko , n.k Vyote hivyo vitakuwezesha kujipanga kwa ufasaha ili kupunguza hasara na muda mrefu wa kufikia mafanikio.
Hii pia inahusika katika aina ya kazi unayotamani kufanya, je ni kwa kiwango gani utahitaji lugha ya kigeni, uwezo wa kutumia teknolojia mpya, kiwango cha elimu , n.k
4.Kubali kuwa tofauti
Wewe na yule mna historia tofauti za maisha, malezi tofauti, tabia tofauti, na hata uwezo wa kufikiri na hisia tofauti. Vyote hivi vinaweza kuchangia katika namna tofauti za kukabiliana na changamoto za kimaisha, na hata katika kupata fursa. Hivyo basi badala ya kuwaza kutaka kuwa kama fulani, tafakari nini wewe kama wewe unaweza kufanya, kiwango gani cha uvumilivu na juhudi kinahitajika ili kufikia malengo yako, na jitahidi kufanya unayotakiwa kufanya kwa juhudi.
Hakuna 'shortcuts' za mafanikio. Na mafanikio ya 'kulazimisha' hayawezi kukuletea furaha ya kweli maishani mwako.
Utakuja kugundua kuwa la msingi sana katika maisha ni kuwa na furaha na amani ya moyoni.
HITIMISHO
Kujitambua mapungufu yako na kuyarekebisha , halafu ukatambua pia mambo uliyo mzuri sana katika hayo, kisha ukazitumia fursa zinazoendana na hayo, kutakufanya ujiweke katika namna nzuri ya kupata dili za kuboresha maisha yako.
Hata hivyo kwakuwa mafanikio ni safari , unapaswa kujipanga kwa kuwa na taarifa sahihi, kuwa na bidii endelevu katika mambo ya msingi, na zaidi sana uweze kujitofautisha na wengine ili uweze kutambulika ubora wako, na hatimaye dili kali zije kwa ajili yako.
business
Tafadhali Share na marafiki story hiiNi jambo lililo wazi kuwa sote tunakumbana na matatizo , ingawaje aina ya matatizo na kiwango ambacho yanatusumbua vinaweza kuwa tofauti.
Hata hivyo, sote tunaweza kutafuta mbinu za kutatua matatizo husika, ingawaje ni kweli mbinu zetu za kutafuta suluhu zinaweza kuwa tofauti.
Katika makala hii kutana na wabunifu Ed na Ross kutoka UK, wanaoendesha biashara yao iitwayo BUY MY FACE.
Ed na Ross kutoka UK
Vijana hawa walianzisha biashara ya kuuza nafasi za matangazo kwa kutumia sura zao. Wanachofanya ni kuandika tangazo kwa uso zao, kisha huzunguka maeneo tofauti tofauti ya mji ili watu waweze kuona tangazo husika.
Na wameshafanya matangazo ya makampuni makubwa kama vile Ernest & Young.
Jionee picha zao hapa


Mambo kadhaa yanayoweza kukufanya kuwa mbunifu:-
1. Ondoa uwoga: Usiogope kuwa wazo lako litakuja kushindwa. Chukulia kuwa hata kama litakuja kushindwa, utakuwa tayari umeshapata uzoefu wa kutengeneza wazo lingine bora zaidi.
2. Usijilinganishe na watu wengine: Usiangalie wengine unao dhani wamekuzidi uzoefu au ujuzi wamefanya nini , kiasi kwamba ukajishusha kuwa eti wewe hauwezi kufikia kuwa na kitu kizuri cha ubunifu.
3. Zingatia Upekee: Kama unataka kufanya UBUNIFU , lakini mawazoni mwako unapata ukinzani wa kutaka kufanya kama fulani, basi ujue hapo kuna tatizo. Sisitiza kuwa na upekee, na upekee tuu ndio utakaoleta maana haswa katika ubunifu wako, hata mbele za wateja. Hata hivyo hii haimaanishi kuwa hautakiwi kuangalia wengine wamefanya nini, hapana, angalia wengine kwa lengo la kujifunza, na kutambua mapungufu.
4. Zingatia kukidhi mahitaji ya binadamu: Ubunifu wako hautokuwa na maana kama haukidhi mahitaji ya watu. Hivyo njia rahisi ya kuanza ubunifu ni kuisoma jamii, kuangalia matatizo yanayoikumba jamii. Sio lazima uangalie mbali sana, waweza hata kutafakari matatizo ambayo yamekuwa yakikutatiza wewe mwenyewe, kisha ukaamua kubuni kitu cha kuleta suluhisho. Fanya uchunguzi kujua wengine wamekumbana na matatizo kama yako.
Mfano mzuri,Drew Houston mwanzilishi wa huduma ya kuhifadhi documents online, DROPBOX anasema alianzisha huduma hiyo baada ya yeye mwenyewe kuwa mpotezaji wa flashdisk wakati akiwa chuoni MIT.
business
Tafadhali Share na marafiki story hiibusiness
Tafadhali Share na marafiki story hiiAMKA NA MBINU ZA KUONGEZA MAUZO YA BIASHARA YAKO. Mzunguko wa fedha ndio damu ya biashara yako. Kama mzunguko huu wa pesa haupo vizuri basi biashara yako itaadhirika na kama mzunguko huu utasimama basi biashara yako itakufa kabisa. Leo tunaangalia eneo muhimu sana la kuhakikisha mzunguko wa fedha kwenye biashara yako unakuwa mzuri. Eneo ili ni mauzo. Mauzo ndio huleta fedha kwenye biashara yako na hivyo kama ukiongeza MAUZO maana yake unaongeza fedha. Japokuwa hii haimanishi kwamba ukiongeza mauzo basi ndo umeongeza faida. Leo tuangalie kwanza kuhusu mauzo ya biashara yako na namna gani ya kuyaongeza. Kabla hatujaona mbinu tano ambazo unaweza kuzitumia kuongeza mauzo kwenye biashara yako naomba nijibu swali muhimu sana ambalo wewe unaweza kujiuliza. Je inawezekana mauzo ya biashara yako kuongezeka....?? Jibu ni NDIO, haijalishi biashara yako ipo kwenye hatua gani, bado una nafasi ya kuongeza mauzo zaidi ya unayoyafanya sasa kikubwa ni wewe kujua mbinu sahihi za kutumia ili uweze kuongeza mauzo yako. Mauzo ya biashara yako yanaweza kuongezeka, sasa unayaongezaje....?? Hapa ndio zinakuja mbinu tano muhimu zinazoweza kutumiwa kuongeza mauzo yako. MBINU YA KWANZA; Uza bidhaa zinazoendana kwa pamoja. Mteja anapokuja kununua bidhaa kwako, tayari amejipanga atanunua bidhaa au huduma fulani. Unaweza kumuuzia bidhaa hiyo na akaondoka unakuwa umepata mauzo ya kile alichokitaka na mambo yanaishia hapo. Ila ukiwa mfanyabiashara mjanja unaweza kumuuzia bidhaa anayotaka na pia ukamjulisha kwamba kuna bidhaa nyingine ambayo inaweza kuwa na matumizi sawa na kile alichochukua. Au endapo bidhaa hizo zitatumika kwa pamoja basi zinaweza kuboresha maisha yake kwa kiasi kikubwa. kwa mfano; kama mtu amenunua nguo, muuzie na viatu na begi la nguo. Kama amenunua kompyuta mwambie kuna vitu muhimu anahitaji kununua ambavyo vitafanya matumizi ya kompyuta yake kuwa mazuri. Kwa mfano kuweza kuhifadhi data zake sehemu tofauti ili zisipotee kompyuta inapopotea. Kama mtu akinunua kitabu kimoja muoneshe na vitabu vingine ambavyo vitampatia maarifa zaidi. Kwemye biashara yoyote unayofanya kuna bidhaa nyingi unazoweza kuuza kwa pamoja. Fanyia kazi hili. MBINU YA PILI; Uza bidhaa yenye uhitaji mkubwa. Ni rahisi kwa mtu kununua tiba kuliko kinga. Ndivyo binadamu tulivyo, kama hakuna tatizo juu ya kitu fulani basi hatuangaiki kupata suluhisho. Ni kazi yako wewe kama mfanyabiashara kuangalia biashara ina matatizo gani ambayo yanaumiza vichwa vya watu na wanatafuta suluhisho lake. Kisha wapatie suluhisho la matatizo yao kupitia biashara yako. Siku njema ya mafanikio
Recent Comments