Select Menu

Slider

Powered by Blogger.

Music

Health

Sports

News

Photos

Documentary

Video

» » KILIMO CHA TANGAWIZI KATIKA WILAYA YA MADABA KINAANZA KUSAMBAA KWA KASI KUTOKANA NA JUHUDI ZA MBUNGE WA JIMBO HILO KWA UAMUZI WAKE WA KUWAINUA WANANCHI http://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

KILIMO cha tangawizi katika Wilaya ya Madaba kinaanza kusambaa kwa kasi kutokana na juhudi za Mbunge wa jimbo hilo, Joseph Mhagama kwa uamuzi wake kuwainua wananchi kiuchumi. Kiongozi huyo amehamasisha kilimo hicho na kugawa tani sita za mbegu ili wananchi waweze kunufaika kwa kuwa zao hilo limepata soko nchini Kenya.

http://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js
Anasema, ni jukumu la viongozi kuhimiza wananchi walime mazao yanayoonesha kuwainua wananchi kiuchumi yakiwemo ya tangawizi, mbaazi, alizeti na maharage. Mhagama anasema, kilimo cha tangawizi kimewezesha wakulima 2,745 kubadili maisha na wapo waliojenga nyumba bora na wengine wamenunua vyombo vya usafiri yakiwemo magari, pikipiki na baiskeli. Anasema, kila siku wafanyabiashara Kenya wanahitaji tani 50 za unga wa tangawizi hivyo ni lazima wananchi wa jimbo hilo wakipende kilimo hicho ili kiweze kuwainua kiuchumi na kufanikisha ustawi wa jamii. “Nimefanya utafiti na kubaini kuwa zao hilo litawaondoa wapigakura wangu kwenye lindi la umasikini,”anasema Mhagama. “Kabla sijawa Mbunge wa Jimbo la Madaba mwaka 2012-2014 nikiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la kiserikali Ruvuma Commercialization and Diversification of Agriculture (RUCODIA) nilifanya utafiti kuhusu shughuli za kilimo na mifugo juu ya mazao yenye tija zaidi, baada ya kubaini umasikini wa kipato unaowakabili wakulima wadogo umekuwa ukichangiwa na kilimo kisichokuwa na tija kwa wakulima mkoani hapa,”anasema. Baada ya kugundua hilo shirika hilo limeelekeza nguvu kwenye mazao ya alizeti na tangawizi kwa kuwa linaamini kwamba linaweza kuinua maisha ya wakulima wadogo na kuwaongezea kipato zaidi badala ya kuendelea kulima kilimo kisichokuwa na tija. Limeunda vikundi vya wakulima wadogo na kuwahamasisha kwa kuwaahidi soko la uhakika la kuuzia mazao yao, kabla ya kupeleka kiwandani kwa kazi ya usindikaji na kuzalisha mafuta ya alizeti yenye ubora. Anasema shirika lilianza na wanachama wakulima 300, lakini mpaka sasa wamefikia wakulima 2,745. Mbegu zilizopandwa wakati huo zilikuwa kilo 10 lakini sasa kuna tani 9,000 hivyo kuonesha kuwa wananchi wamehamasika kujikomboa kiuchumi. Mhagama anasema, wananchi wanatakiwa wazalishe kwa wingi mazao muhimu kwa kiuchumi kwa wilaya ya Madaba. RUCODIA ina jukumu la kuhakikisha mazao ya wakulima yananunuliwa. Shirika hilo limenunua tani zaidi ya 850 za alizeti kwa bei ya Sh 450 kwa kilo moja na kuwawezesha kuwalipa zaidi ya Sh 502,500,000. Wameweza pia kununua tani zaidi ya 600 za tangawizi kwa bei ya Sh 1,000 kwa kilo na wameweza kuwalipa wakulima wa zao hilo zaidi ya Sh milioni 500. Mratibu wa Rucodia, Ladislaus Bigambo anasema, tangawizi ni kiungo ambacho sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambayo huonekana kama mizizi ya mmea. Anasema, asili ya zao hilo ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China. Bigambo anasema zao hilo linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica na kwa hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Ruvuma Wilaya ya Madaba, Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro. Anasema tangawizi hutumika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji ikiwemo chai, soda, juisi, vilevi na vyakula mbalimbali kama vile mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, na achari. Bigambo anasema, zao hilo hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza dawa ya tiba ikiwemo ya meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi wakati mwingine pia hutumika katika vipodozi kama poda. Zao hilo hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi na huhitaji mvua kiasi cha mm. 1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25 na hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji. Mkulima wa zao hilo kutoka Mkongotema, Menas Mgaya anasema, elimu inayotolewa na RUCODIA imewawezesha kupiga hatua za kimaendeleo kwa kulima mazao yenye tija na yenye uhakika wa soko kwani wamefanikiwa kufanya hivyo baada ya kuwahamasisha na kuitikia mwito wao na kuunda kikundi chao ambapo kupitia kikundi hicho wamekuwa wakiuza mazao yao na kujipatia fedha Mgaya anasema, kupitia kilimo hicho sasa wana uhakika wa chakula na watu wanazimudu gharama za huduma muhimu kama elimu ya watoto, afya na makazi bora. Kwa mujibu wa mkulima huyo, awali walikuwa wanashindwa kuzitumia vyema maliasili kama misitu , ardhi, maji na hali ya hewa iliyopo wilayani mwao hivyo watu wengi wakashindwa kuwa na sauti katika jamii au kushiriki katika mipango, ufuatiliaji na uamuzi na kubaki wanyonge kutokana na umasikini. “Laiti kama tungalitumia mbinu za kijasiriamali, au kilimo chenye manufaa tungekuwa mbali sana kiuchumi,”anasema Mgaya. “Tungekuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kumudu maisha, tena kwa kujiamini kuliko ilivyo sasa kama kweli viongozi wetu wangekuwa wanatumia utafiti sahihi wa kuondokana na umasikini katika maeneo yetu kuliko kuendelea kufanya maisha ya kilimo au kiujasiriamali bila utafiti,”anasema. Mkulima kutoka Magingo, Osmund Njelekela anasema, zao la tangawizi ni mkombozi kwa wakulima wa eneo hilo kwa kuwa limewaondoa kwenye unyonge na umasikini. Njelekela anasema, siku za mwanzo hali ya umasikini kwenye kaya zao ilikuwa imekithiri na kuwafanya hali hiyo kuwakosesha elimu na huduma nyingine kwa watoto na wakashindwa kumudu kuzihudumia familia. Wakulima wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kudhamiria kuinua uchumi wa mtu wa kati kwa kutoa mbegu za tangawizi na vitendea kazi. Wanasema kukiwepo rasilimali ardhi, na watu wakipewa nyenzo Tanzania haitakuwa miongoni mwa nchi zinazolalamika na umasikini kwa kuwa mito ipo, maziwa yapo pamoja na mvua za kutosha. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba, Vastus Mfikwa anasema, kwa kushirikiana na Mbunge wameweza kuzitembelea kata zote na kuainisha vipaumbele vya kuwakomboa wananchi kiuchumi kielimu na kiafya. Mfikwa anasema Mbunge ametoa mbegu tani sita za tangawizi, ameweza kugawa pikipiki 3 pamoja na baiskeli 6 kwa ajili ya walemavu na baiskeli nyingine kupeleka katika kituo cha afya Madaba ili iweze kusaidia wagonjwa wasiojiweza kutembea kutoka wodi moja hadi nyingine. Anasema, kwa muda mrefu Mbunge Mhagama amekuwa akishirikiana zaidi na wananchi kwa kuanzisha miradi kwa wakulima wadogo ikiwa ni pamoja na kilimo cha ufuta, alizeti na tangawizi hivyo ameahidi kushirikiana na madiwani wenzake kuhakikisha jimbo hilo linakua kwa kasi kiuchumi. Kwa mujibu wa Mfikwa, Halmashauri ya Madaba ina jimbo jipya na ina wananchi wenye vipato vidogo hivyo wanahitaji kujengewa uwezo zaidi ambao utamwezesha kila mwananchi ambaye ni mkulima kuwa na kipato kisichopungua Sh 300,000 kwa mwezi. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba, Robeti Mageni amewataka wadau wa maendeleo kujitokeza kwa wingi ili waweze kushirikiana kuipaisha kiuchumi wilaya hiyo. Anatoa changamoto kwa wazawa wa eneo hilo ambalo wapo ndani na nje kutumia fursa za kiuchumi zilizopo wilayani humo na wajitahidi kila moja kwa nafasi yake kuwezesha maisha yenye

About Arusha99

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply