Jennifer Mgendi alizaliwa tarehe 02 May, 1972 hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam, (kwa sasa ana miaka 44), mama yake akiwa Mwendapelu Nalaila na baba akiwa Fanuel Mgendi, amesoma shule ya msingi Mgulani, Shule ya sekondari Kisutu, Chuo cha Ualimu Korogwe na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Jennifer Mgendi amewahi kufanya kazi katika Shule ya Sekondari Handeni, Shule ya Sekondari Tambaza, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Chuo Kikuu cha afya Muhimbili. Mwaka 2007 aliacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri katika kazi za sanaa na Muziki wa Injili. Safari yake ya muziki wa injili ilianza rasmi mwaka 1995 aliporekodi albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la NINI?. Mpaka sasa ana album nane, UKARIMU WAKE(2000), NIKIONA FAHARI(2001), YESU NAKUPENDA(2003), MCHIMBA MASHIMO(2016), KIU YA NAFSI(2009), DHAHABU (collection- 2012), HONGERA YESU na WEMA NI AKIBA. Jennifer Mgendi alifunga pingu za maisha mwaka 1998 na Dr. Job Chaula ambaye amefanikiwa kupata nae watoto watatu ambao ni Jotham, Jeftah na Joan. Filamu yake ya kwanza kuiandaa na kuigiza ni Joto la roho iliyotoka mwaka 2004 na aliyomshirikisha Mwimbaji Bahati Bukuku na ndiyo iliyozaa wimbo wa Nalia. Wimbo wa Nalia uliandaliwa mahususi kwa ajili ya kutumika kwenye filamu hiyo ambayo inazungumzia maswala mbalimbali kuhusu mahusiano na inafaa sana kwa kufundishia vijana. Filamu nyingine alizowahi kuigiza ni pamoja na Pigo la faraja (2005), Teke la mama (2009), Wema ni akiba na zinginezo. Source: JenniferMgendi.Com
Tagged with: Gospel
About Arusha99
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments