tunauza sabuni za maji na dawa za usafi tunauza kwa bei ya jumla na rejareja pia tunatafuta vijana wa kutafuta order bidhaa zetu watalipwa kwa commission wasiliana nasi kwa no 0753606603
entrepreneurs
Tafadhali Share na marafiki story hii
Dawa hii hutengenezwa kwa kutumia malighafi tatu ikiwemo sabuni ya maji, maji yenyewe pamoja na vinegar.
Katika kutengeneza dawa hii unapaswa kuandaa chombo chenye ukubwa wa plastik ambapo utaweka maji lita kumi,sabuni ya maji lita moja pamoja na vinegar lita tatu.
Baada ya mchanganyiko huo utakoroga kwa dakika zisizopungua ishirini na tano na dawa yako itakuwa tayari kwaajili ya matumizi.Asante.
entrepreneurs
Tafadhali Share na marafiki story hii
Tumekuwa mala nyingi na utaratibu wa kununua Air fresh na bidhaa nyingine kutoka nchi za nje kwa vigezo kuwa hatuwezi kutengeneza wenyewe au bidhaa zetu sio bora.Hapa nakuletea jinsi ambavyo unaweza kujitengenezea Air fresh yako mwenyewe na kuifanya nyumba yako kuwa na harufu nzuri tu.
Ili bidhaa yako ikamilike unahitaji baadhi ya vitu kama mvuke ambao umepoa.Hapa nina maanisha kuwa mvuke unapopoa untengeneza maji kwahiyo tunatakiwa kuwa na maji lakini lazima maji hayo yatokane na mvuke.
Unaweza kutengeneza maji hayo kwa kuchemsha maji kutunia pipa moja lililofungwa pande zote na kuwa na mrija au mpira unaotoka katika pipa hilo kuelekea kwenye pipa lingine ambalo liko pembeni.
Kwa mfumo huo maana yake ni kuwa mvuke kutoka pipa A unaotokana na kuchemka kwa maji utaelekea pipa B.Hakikisha unapata maji ya kutosha.
Uache mvuke katika pipa B upoe halafu anza kutengeneza kwa kuchukua maji lita ishirini uchanganye na harufu vijiko vinne vya chakula na ukoroge kwa dakika zisizopungua ishirini na tano.Ongeza tena maji lita kumi na ukoroge kwa dakika tano.Hapo Airfresh yako itakuwa tayari na weka kwenye containers kwaajili ya matumizi.
entrepreneurs
Tafadhali Share na marafiki story hii
Moja kati ya mahitaji makubwa ya watu ikiwemo wafanyabiashara za mama lishe,mabucha na nyingine,ni sabuni ya kunawia.Kutokana na mahitaji makubwa waliyonayo watu na kukosekana kwa bidhaa hiyo wahitaji hujikuta wakitumia sabuni ambazo hazikutengenezwa kwa kazi hiyo kama sabuni za unga,shampoo na sabuni za vipande ambazo huwasababishia madhara bila kujijua.
Leo katika somo letu tutajifunza jinsi ya kutengeneza sabuni za kunawia mikono.fuatana nami mwanza mpaka mwisho.
MAHITAJI;
.Sulphonic acid
.soda ash
.maji yaliyochujwa vizuri
.pafyum
.Rangi yoyote inayovutia
.sless
.Chumvi
JINSI YA KUTENGENEZA.
Andaa vizuri chombo chako kwaajili ya kutengenezea sabuni yako kama ndoo au pipa pamoja na kuandaa malighafi zako huku ukizingatia usafi.
Tanguliza kumimina ssulphonic acid vijiko vitano vya chakula kwenye chombo chako.
Endelea kuweka soda ash iliyochanganywa na maji vijiko vitatu vya chai.
Weka maji lita tano ukifuatiwa na sless robo lita,chukua pafyum yoyote na uweke kijiko kimoja na nusu cha chai.
Ongeza rangi kijiko kimoja cha chai na uanze kunyunyizia chumvi ambayo huleta uzito na kufanya sabuni yako isiharibike na kukaa muda mrefu.
Koroga vyote kwa pamoja kwa muda wa dakika ishirini na sabuni yako itakuwa tayari.
entrepreneurs
Tafadhali Share na marafiki story hii
Karibu tena msomaji kwenye somo letu kama tulivyozoea kupata masomo haya ya kujikwamua na umaskini.leo nakuletea somo ambalo litakua la mwisho kwa masomo amboyo utayapata bure na atakaetaka masomo zaidi basi atanipigia simu kwenye namba inayoonekana pembeni na tutapatana kwa malipo kidogo tu.
Somo la leo linahusu jinsi ya kutengeneza sabuni za unga.
MAHITAJI.
.Optical bytina.
.sodium carbonate.
.sulphonic acid.
.Sodium sulphate.
.Hoda ash.
.Hydrogen peroxide.
.Rangi.
.Perfume.
JINSI YA KUTENGENEZA.
Andaa chombo chochote kinachoendana na wingi wa sabuni unayotaka kutengeneza na anza kutengeneza kwa kufuata hatua zifuatazo.
.weka sodium carbonate kwenye chombo ulichoandaa kg2 na nusu.
.Baada ya hapo weka optical bytina vijiko kumi(10)vya chakula.
.halafu weka sodium sulphate vijiko vitano vya chakula.
.weka soda ash kg7 na ukoroge kwa muda wa dakika kumi.
HATUA YA PILI.
.Sulphonic acid kilo 2 na nusu.
.nausa vijiko 15 vya chakula.
.Hydrogen peroxide kama ni ya unga weka kilo mbili kama ya maji weka lita mbili.
.rangi vijiko vitano vya chakula.
. changanya na perfume vijiko sita vya chakula.
.baada ya mchanganyiko huo anika kwenye kuvuli kwa kuwa juani inaweza kuyeyuka.sabuni yako itakauka kwa kujiachia.Kusanya weka kwenye mifuko tayari kwa kuuza.
ONYO:Baadhi ya malighafi ni acid kwahiyo umakini unatakiwa wakati wa kutengeneza,hakikisha mikono yako imelindwa kwa gloves na usishike acids au kula wakati unafanya kazi.Tafadhari watu wazima ndio wafanye kazi hii.KAZI NJEMA KUPAMBANA NA UMASKINI.
entrepreneurs
Tafadhali Share na marafiki story hii
UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA MICHE
A)MAHITAJI:- Kostik soda ya unga au ya mabonge
Maji safi
Mafuta ya mise/pamba/nazi/mawese n.k
Rangi ya kutengenezea sabuni za miche(blue/pink/kijani n.k
Marashi upendayo lemon/apple n.k
Tanbihi:kama unata kutengeneza sabuni za tiba(virutubisho)utahitaji kuwa na kirutubisho unacho taka kutumia kwa mf:Aloe Vera/Ubuyu/Papai/Mwarobaini n.k
Box la kutengenezea sabuni na vibao vya kukatia sabuni vyenye ukubwa wa mche wa sabuni.
Ndoo kubwa za maji angalau 3 na ndoo ndogo 3,conduse ya plastiki kwa ajili ya kukorogea.Sodium Siliket,magadi soda,Hydrometa nzito pamoja na meza ya kukatia sabuni.
Kanuni:-kostik kg 1
Maji lita 3
Mafuta lita 6
Sodium siliket grm 500
Magadi soda vijiko vikubwa vya chakula 10
Rangi kijiko 1 cha chakula
Pia utahitaji eneo la kufanyia kazi pamoja na rasilimali watu angalau wawili.
Loweka kostik soda kwa masaa 24,kasha ikoroge na uipime nguvu yake kwa kutumia hydrometa iwe bomee 25-30bm
Ikiwa imezidi bm 30 haifai kwa matumizi ya binadamu ipunguze nguvu kwa kuongeza maji kiasi na upime tena,chukua ndoo ndogo ya maji na uweke mafuta,soda ash,sodium siliket,manukato na uchukue mafuta kidogo uweke kwenye spray(kiasi cha nusu lita)na uchananye na rangi au virutubisho na ukoroge vizuri baada ya kukoroga vizuri changanya na kostik soda koroga tena mpaka ichanganyike vizuri weka nailoni laini kwenye box kuzuia mchanganyo wa sabuni kumwagika(kuvuja) anza kupulizia rangi kwenye box na endelea kumimina mkorogo(mchanganyo wa sabuni kidogo kidogo huku ukiendelea kupulizia rangi kwa awamu mpaka mwisho mwisho weka contena la sabuni(box)kwenye sehemu nzuri ambapo ardhi imenyooka na usubiri kwa masaa 24 bonge la sabuni litakuwa tayari kukatwa na ili sabuni ikauke vizuro anika chini kwenye sakafu lakini tanguliza magazeti na chumba kisiwe chenye kuingiza mwanga wa jua.
entrepreneurs
Tafadhali Share na marafiki story hii
Subscribe to:
Posts (Atom)
Recent Comments