Kuna hii biashara ya mahindi ya kuchoma (maarufu kama gobo). Unaweza kulima kwa kutumia mtaji kidogo na kupata sarafu za kutosha. Angalia mchanganuo ufuatao: kukodi shamba ekari moja wastani wa tsh 50,000/=, kulima 30,000/=, kupalilia 30,000/=, mbolea mifuko mi-3, tsh 150,000/=, madawa wastani tsh 50,000/=; Jumla kuu ni tsh. 310,000/=. Gharama hii hauitoi mara moja bali ni kidogo kidogo kutegemea hatua husika. Mahindi huchukua wastani wa siku 90 (miezi mitatu) tangu kupanda hadi kugoboa (yaani kuvuna haya mahindi mabichi). Unaweza kupanda kwa kutumia mvua au kutumia umwagiliaji mahali popote Tanzania. Kwa ekari moja ukilima kwa kuzingatia utaalamu una uhakika wa kuvuna kuanzia mahindi 9,800. Hindi moja huuzwa kwa tsh. 150/= hadi 250/=, kutegemea hali ya soko kwa bei ya jumla. Ukikokotoa utaona kuwa kwa ekari moja unaweza kupata tsh. 1,470,000/= kwa kadirio la chini na tsh. 2,450,000/= kwa kadirio la juu. Ukitoa gharama za uendeshaji (za moja kwa moja) unaweza kukunja faida ya hadi tsh 2,140,000/= kwa kadirio la juu. Ukilima eka 5, una uhakika wa faida ya tsh milioni 10.7. Je, ukilima misimu kadhaa, bado utashindwa kujenga nyumba ya maana au kuwa na maisha yenye unafuu? Bila shaka utaweza! Unachohitaji wewe ni mambo yafuatayo: utayari, uthubutu, kuwa-up-to-date kwa taarifa za misimu na masoko na uwe ni mtu wa kufuatilia fursa na kujifunza. Fursa zipo 'bwerere', kama una 'allergy' na kilimo tafuta na ujifunze fursa nyinginezo; LAKINI; mtu YEYOTE anaposema fedha ni ngumu, kiukweli anakuwa hayupo "serious" kabisa na haya maisha! http://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js
agriculture
Tafadhali Share na marafiki story hii HIVI ndivyo anavyosema mkulima wa nyanya kutoka katika kijiji cha Mangalali, bwana Paschal Sichalwe baada ya kuanza kubadili mbinu za kilimo za kizamani na kuanza kutumia mbinu za kisasa alizozipata kupitia mafunzo yanayotolewa na mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI)
http://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js
Mjasiriamali huyu mdogo anaelezea namna ambavyo mradi wa MUVI ulivyoonesha njia ya kuelekea kwenye mafanikio kwa kutoa mafunzo ya kilimo bora, kuboresha njia za mawasiliano baina yao pia jitihada zinazofanywa katika kuwaunganisha na masoko mbalimbali ya ndani na nje ya nchi Mradi wa MUVI kwa kushirikiana na viongozi wa shirikisho la wakulima wa nyanya wamefanya ziara za ndani na nje ya nchi katika harakati za kutafuta masoko zaidi, katika hatua za awali uongozi huo umefika nchini Kenya, Malawi na hatimaye Zambia hii ikiwa ni kwa upande wa masoko ya nje Masoko ya ndani, mradi wa MUVI ambao pia umeimarisha kitengo chake cha biashara na masoko wameangalia masoko ya ndani ya nchini na kugundua kuwa kinachosababisha nyanya kushuka bei ni kukosekana kwa taarifa za biashara na masoko kutoka katika ngazi zote. Katika kutatua tatizo hilo tayari mtandao wa mawasilano kutoka mikoa yote Tanzania zitakuwa zikipatikana ili wazalishaji wa nyanya waweze kufahamu soko liliko. Wakulima wanapopata taarifa za biashara na masoko inakuwa rahisi kwao kufanya maamuzi ya soko. Pia matumizi ya mbao za matangazo kwa kushirikiana na redio country fm88.5 fm na Uplands redio 89.0 fm wajasiriamali vijijini wataweza kupata taarifa za biashara na masoko. Aidha bwana Sichalwe ambaye ameanza kuvuna nyanya alizopanda kitaalamu akitumia mbegu bora aina ya Eden inayozalishwa na Kampuni ya Monsanto anasema kuwa ameanza kuona faida kwani mara ya kwanza ameweza kuchuma tenga 33 ilihali msimu mzima uliopita katika shamba hilo hilo lenye ukubwa wa nusu ekari kwa ujumla alivuna kiasi cha tenga 56 tu. “Msimu uliopita nilitumia mbegu aina ya ONXL katika shamba la nusu ekari michumo yote nilipata tenga 56 tu lakini sasa mchumo mmoja nimewezakuchuma tenga 33 na nategemea kuchuma kiasi cha tenga 26 katika mchumo wa pili.” anasisistiza Sichalwe. Msimu uliopita nilitumia kiasi cha shilingi 532,800 ikiwa ni gharama nzima ya uzalishaji kwa upande wa pembejeo pamoja na nguvukazi,mapato ilikuwa 606000, msimu huu nimetumia kiasi cha shilingi 570,900 kwa ajili ya pembejeo na nguvu kazi nategemea kupata kiasi cha shilingi 1,045,000 Kwa mtizamo wa haraka haraka, bwana Sichalwe ameanza kuona faida katika kilimo cha nyanya kufuatia mchanganuo huo alioufanya. Sichalwe ambaye pia pamoja na zao la nyanya hujishughulisha na kilimo cha alizeti na mahindi, katika hatua nyingine amewezakuimarisha biashara ya kuuza bidhaa ndogondogo kwenye kibanda chake ambapo pia anaamini kuwa kuna siku atakuwa mjasiriamali mkubwa. Awali Sichalwe alikuwa akilima kwa mazoea bila kutunza kumbukumbu kuanzia uzalishaji hadi sokoni lakini baada ya mradi wa MUVI kupisha hodi kijijini kwake na kufundishwa kilimo cha kibiashara na njia rahisi ya kuandaa mpango biashara sasa ameweza kutunza taarifa zake za kilimo tangu hatua ya mwanzo hadi mwisho, hapo ndipo anapoweza kubaini mapato na matumizi katika shughuli nzima. “Wajasiriamali wengi wanasahau kuweka kumbukumbu za uzalisha katika shuguli zao wanazofanya kila siku, mali bila daftari hupotea bila kujua,kila unachofanya inakupasa uandike, kuna wengine pia hujisahau wao wenyewe, mfano akipalilia nyanya mwenyewe au akipanda hujisahau katika kipengele cha malipo ile ni nguvu kazi inapaswa kulipwa na hili linawezekana kama utakuwa umeandika”anasema. Katika hatua nyingine Sichalwe anaamini kuwa baada ya kupata mavuno mengi na yakutosha msimu huu anatarajia kuanza kilimo cha umwagiliaji ambacho anaamini kuwa kitamkomboa zaidi. Pamoja na mambo mengine Sichalwe anampango wa kuimarisha kilimo cha ufugaji kwani tayari amenunua mbuzi 5 mara baada ya kuuza nyanya. Idadi hiyo anaona kuwa haitoshi hivyo anategemea kuongeza kiasi hicho hadi kufikia mbuzi 20. Si hapo tu Sichalwe anaamini pia kwa kuzingatia mbinu za kisasa alizozipata kupitia mradi wa MUVI kufikia mwishoni mwa mwaka atakuwa amenza ujenzi wa nyumba ya kisasa ya kuishi. Katika kuhakikisha kuwa Sichalwe na wajasiriamali wengine wanaozalisha nyanya kijijini hapo wanapata mafanikio, mradi wa MUVI umemtuma ofisa masoko wa mradi huo kuzungumza na na wakulima wa nyanya katika hali ya kuwaondoa hofu hususani kwenye kipengele cha masoko. Akizungumza na wajasiriamali wa Mangalali hivi karibuni muda mfupi mara baada ya kuunda kamati ya biashara na masoko, Ofisa masoko wa mradi, bwana Fredy Mumbuli amesema, wakulima wanategemea zaidi soko la Kariakoo na Ilala.Wafanyabiashara hawa huwa wanakimbilia katika masoko haya kwa kukosa taarifa nzuri za masoko. “wajasiriamali hupeleka nyanya kwa wingi katika masoko hayo kwa kukosa taarifa sahihi za masoko hali inayoplekea kushuka kwa bei ya bidhaa husika,wakulima wote nchini wakishavuna hufikiria kuuza bidhaa zao Dar es salaam jambo ambalo si sahihi hata kidogo.”alisema Mumbuli. na kuzidi kubainisha kwamba kuwa kuna wakati kunakuwepo na uhitaji mkubwa wa nyanya Morogogo, Arusha au Dodoma na hata wakati mwingine Iringa Mkulima anayezalisha nyanya Morogoro akipata taarifa za soko zuri la nyanya Iringa anaruhusiwa kufanya biashara vivyo hivyo na kwa upande wa mkulima wa Arusha, Kilimanjaro na mikoa mingine inayolima zao hilo. Hili litawezekana mara baada ya kuimarisha njia za upashanaji habari kupitia vyombo vya habari na mbao za matangazo ambazo tayari mradi wa MUVI umejenga katika kata 16 mkoani Iringa na Njombe. Kitengo cha habari na mawasiliano kitakuwa kikifanya kazi kwa ushirikiano mzuri na kitengo cha biashara na masoko katika kuwapatia wakulima taarifa za biashara na masoko.
agriculture
Tafadhali Share na marafiki story hiiagriculture
Tafadhali Share na marafiki story hiiORA CHA PILIPILI HOHO Jina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha. Kilimo hiki kinaendeshwa na wakulima wadogo katika maeneo yenye ukubwa wa kati ya hekta 0.2-0.4 pia kuna maeneo ya wakulima wakubwa wenye hekta kati ya 2-20. Wakulima hao hujishughulisha na kilimo cha zao hilo kwa njia ya mkataba na kampuni hiyo. Hoho hutumika katika kutengeneza rangi za asili za vyakula ambazo kwa sasa hupendwa zaidi kuliko zile zinazotokana na kemikali na pia huongeza ladha na harufu katika vyakula. Hivyo hutumika katika viwanda vya kusindika vyakula, kwa mapishi ya nyumbani na hata katika viwanda vya vipodozi kama rangi ya mdomo, uso n.k. Ina virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kama madini ya chuma, vitamin A na C. 
http://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js
2.0 TABIA YA MMEA Hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene kiasi la duara pia linaweza kuwa lililochongoka,. 3.0 ENEO NA HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO Hoho hustawi vema katika maeneo ya usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 2,000 yenye mvua ya wastani wa mm.600-1,250 na wastani wa joto la nyuzi za sentigredi 21 hadi 24. Udongo wa tifitifu wenye rutuba, usiotuamisha maji na wenye hali ya uchachu (pH) kati ya 5.0-6.5 hufaa zaidi. Umwagiliaji ni muhimu pale mvua inapokuwa chache. 4.0 UZALISHAJI 4.1 UTAYARISHAJI WA KITALU Chagua eneo katika ardhi isiyo na mtelemko mkali na yenye rutuba ya kutosha. Ardhi iwe imepumzishwa bila kuoteshwa mazao ya jamii ya pilipili, biringanya, nyanya, n.k. ili kuepukana na mashambulizi ya wadudu na magonjwa. Tayarisha kitalu kabla ya msimu wa mvua. Andaa vizuri matuta manne yenye urefu wa wastani wa mita 10 kila moja na upana wa mita moja (1) ili kustawisha miche inayotosha ekari moja. Acha njia ya nusu mita kati ya tuta na tuta. Mwagilia maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu na endelea kunyweshea kulingana na hali ya hewa na hali ya udongo. Sia mbegu kwenye, mstari, nafasi kati ya mstari na mstari ni sm 10 na kina cha sm1. Kiasi cha mbegu cha nusu kilo kinatosha eneo la hekta moja. Weka matandazo kwenye kitalu au tumia nailoni nyeusi ili kuhifadhi unyevunyevu na kuzuia uotaji wa magugu. 4.2 UTAYARISHAJI WA SHAMBA Shamba lilimwe vizuri na kuweka matuta ili kuhifadhi unyevunyevu na kurahisisha umwagiliaji. Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja.  4.3 UPATIKANAJI WA MBEGU Mbegu ambazo hutumika ni chotara ambazo huuzwa kwenye maduka ya pembejeo za kilimo nchi nzima. Haishauriwi kutumia mbegu kutoka zao la msimu uliopita kwani ubora wa paprika utaharibika na hivyo kuharibu soko unashauriwa kununua mbegu bora. 4.4 UPANDAJI Mbegu huoteshwa na kukuzwa kitaluni kwa muda wa wiki 6-8 na miche hupandikizwa shambani ikiwa na urefu wa sm.6-10. Mwagilia maji kitaluni kabla ya kuhamisha miche. Panda shambani kwa nafasi ya sm.75-90 kati ya miche kwa sm.90-105 kati ya mistari, wastani wa miche 12,500 itapatikana kwa hekta. Weka samadi shambani tani 25-37 kwa hekta wiki 1-2 kabla ya kupandikiza miche, au kilo 560-670 za NPK (mbolea ya viwandani) kwa hekta kwa uwiano wa 4:7:7 katika udongo usio na rutuba ya kutosha. ITALIAN PAPRIKA  5.0 KUHUDUMIA SHAMBA Palizi ifanyike mara magugu yanapotokea shambani. Umwagiliaji maji ufanyike kama ilivyo kwa mazao mengine kama nyanya. Tumia mbolea kiasi cha kilo 140 za SA au CAN kwa hekta hasa wakati mmea inapotoa matunda ili kupata matunda makubwa na kuvuna kwa muda mrefu (hadi miezi 10). 6.0 MAGONJWA NA WADUDU Wadudu • Funza wa vitumba • Vidukari • Kidomozi (Leaf miner) Kudhibiti: Tumia dawa aina ya permethrin Magonjwa • Kuoza mizizi • Mnyauko wa majani • Batobato Kudhibiti: Choma nyasi kwenye kitalu kabla ya kusia mbegu. Badilisha mazao yasiyo ya jamii ya pilipili. 7.0 UVUNAJI Matunda ya kwanza huwa tayari kuvunwa kuanzia miezi 2-3 baada ya kupandikizwa; matunda yaliyokomaa vizuri na kuwa na rangi nyekundu ndiyo huvunwa. Matunda 30-80 hupatikana kwa mmea mmoja. Ubora wa hoho huongezeka kutegemeana na kiwango cha rangi yake ikiwa ni nyekundu njano au kijani. Mazao kiasi cha tani 3.5 kwa hekta hupatikana. Baada ya kuvuna mwagilia maji, piga dawa (kama ni muhimu) na weka mbolea kuongeza uzalishaji unaofuata. 8.0 USINDIKAJI Hoho huuzwa ikiwa bado fresh tofauti na jamii nyingine za pilipili ambazo zinaweza kukaushwa na kusindikwa kasha kuuzwa baadae.  9.0 SOKO LA PAPRIKA Soko la hoho lipo nchi nzima kwenya masoko makubwa na hata magengeni, hoho hutumiwa zaidi kama kiungo cha kupikia mapishi mbali mbali au kutia kwenye kachumbari. Tatizo kubwa wanalokabiliana nalo wakulima ni kutokuwa na soko la uhakika ndani na nje ya nchi, mazao huweza kuoza shambani au njiani kutokana na tabu ya usafiri hasa vijijini ambapo mvua zikinyesha barabara hazipitiki kwa urahisi Kuna aina ya pilipili isiyo kali kama hoho lakini ni ndefu kama pilipili za kawaida ijulikanayo kama PAPRIKA ambayo ina soko kubwa nje ya nchi. Zao hili kwa sasa huzalishwa kwa msukumo wa kampuni ya kigeni ya Hispania inayoitwa Tanzania Spices Ltd iliyopo mkoani Iringa  10.0 GHARAMA YA UZALISHAJI WA HEKTA MOJA: Mbegu Tshs. 24,000 /- Vibarua 200,000/- Mbolea(mboji/samadi) 300,000/- Madawa 100,000/- Jumla 624,000/- MAPATO: Kilo 3,500/- X 800/- 2,800,000/-
agriculture
Tafadhali Share na marafiki story hiiKILIMO cha tangawizi katika Wilaya ya Madaba kinaanza kusambaa kwa kasi kutokana na juhudi za Mbunge wa jimbo hilo, Joseph Mhagama kwa uamuzi wake kuwainua wananchi kiuchumi. Kiongozi huyo amehamasisha kilimo hicho na kugawa tani sita za mbegu ili wananchi waweze kunufaika kwa kuwa zao hilo limepata soko nchini Kenya.
http://pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js
Anasema, ni jukumu la viongozi kuhimiza wananchi walime mazao yanayoonesha kuwainua wananchi kiuchumi yakiwemo ya tangawizi, mbaazi, alizeti na maharage. Mhagama anasema, kilimo cha tangawizi kimewezesha wakulima 2,745 kubadili maisha na wapo waliojenga nyumba bora na wengine wamenunua vyombo vya usafiri yakiwemo magari, pikipiki na baiskeli. Anasema, kila siku wafanyabiashara Kenya wanahitaji tani 50 za unga wa tangawizi hivyo ni lazima wananchi wa jimbo hilo wakipende kilimo hicho ili kiweze kuwainua kiuchumi na kufanikisha ustawi wa jamii. “Nimefanya utafiti na kubaini kuwa zao hilo litawaondoa wapigakura wangu kwenye lindi la umasikini,”anasema Mhagama. “Kabla sijawa Mbunge wa Jimbo la Madaba mwaka 2012-2014 nikiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la kiserikali Ruvuma Commercialization and Diversification of Agriculture (RUCODIA) nilifanya utafiti kuhusu shughuli za kilimo na mifugo juu ya mazao yenye tija zaidi, baada ya kubaini umasikini wa kipato unaowakabili wakulima wadogo umekuwa ukichangiwa na kilimo kisichokuwa na tija kwa wakulima mkoani hapa,”anasema. Baada ya kugundua hilo shirika hilo limeelekeza nguvu kwenye mazao ya alizeti na tangawizi kwa kuwa linaamini kwamba linaweza kuinua maisha ya wakulima wadogo na kuwaongezea kipato zaidi badala ya kuendelea kulima kilimo kisichokuwa na tija. Limeunda vikundi vya wakulima wadogo na kuwahamasisha kwa kuwaahidi soko la uhakika la kuuzia mazao yao, kabla ya kupeleka kiwandani kwa kazi ya usindikaji na kuzalisha mafuta ya alizeti yenye ubora. Anasema shirika lilianza na wanachama wakulima 300, lakini mpaka sasa wamefikia wakulima 2,745. Mbegu zilizopandwa wakati huo zilikuwa kilo 10 lakini sasa kuna tani 9,000 hivyo kuonesha kuwa wananchi wamehamasika kujikomboa kiuchumi. Mhagama anasema, wananchi wanatakiwa wazalishe kwa wingi mazao muhimu kwa kiuchumi kwa wilaya ya Madaba. RUCODIA ina jukumu la kuhakikisha mazao ya wakulima yananunuliwa. Shirika hilo limenunua tani zaidi ya 850 za alizeti kwa bei ya Sh 450 kwa kilo moja na kuwawezesha kuwalipa zaidi ya Sh 502,500,000. Wameweza pia kununua tani zaidi ya 600 za tangawizi kwa bei ya Sh 1,000 kwa kilo na wameweza kuwalipa wakulima wa zao hilo zaidi ya Sh milioni 500. Mratibu wa Rucodia, Ladislaus Bigambo anasema, tangawizi ni kiungo ambacho sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambayo huonekana kama mizizi ya mmea. Anasema, asili ya zao hilo ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China. Bigambo anasema zao hilo linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica na kwa hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Ruvuma Wilaya ya Madaba, Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro. Anasema tangawizi hutumika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji ikiwemo chai, soda, juisi, vilevi na vyakula mbalimbali kama vile mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, na achari. Bigambo anasema, zao hilo hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza dawa ya tiba ikiwemo ya meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi wakati mwingine pia hutumika katika vipodozi kama poda. Zao hilo hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi na huhitaji mvua kiasi cha mm. 1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25 na hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji. Mkulima wa zao hilo kutoka Mkongotema, Menas Mgaya anasema, elimu inayotolewa na RUCODIA imewawezesha kupiga hatua za kimaendeleo kwa kulima mazao yenye tija na yenye uhakika wa soko kwani wamefanikiwa kufanya hivyo baada ya kuwahamasisha na kuitikia mwito wao na kuunda kikundi chao ambapo kupitia kikundi hicho wamekuwa wakiuza mazao yao na kujipatia fedha Mgaya anasema, kupitia kilimo hicho sasa wana uhakika wa chakula na watu wanazimudu gharama za huduma muhimu kama elimu ya watoto, afya na makazi bora. Kwa mujibu wa mkulima huyo, awali walikuwa wanashindwa kuzitumia vyema maliasili kama misitu , ardhi, maji na hali ya hewa iliyopo wilayani mwao hivyo watu wengi wakashindwa kuwa na sauti katika jamii au kushiriki katika mipango, ufuatiliaji na uamuzi na kubaki wanyonge kutokana na umasikini. “Laiti kama tungalitumia mbinu za kijasiriamali, au kilimo chenye manufaa tungekuwa mbali sana kiuchumi,”anasema Mgaya. “Tungekuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kumudu maisha, tena kwa kujiamini kuliko ilivyo sasa kama kweli viongozi wetu wangekuwa wanatumia utafiti sahihi wa kuondokana na umasikini katika maeneo yetu kuliko kuendelea kufanya maisha ya kilimo au kiujasiriamali bila utafiti,”anasema. Mkulima kutoka Magingo, Osmund Njelekela anasema, zao la tangawizi ni mkombozi kwa wakulima wa eneo hilo kwa kuwa limewaondoa kwenye unyonge na umasikini. Njelekela anasema, siku za mwanzo hali ya umasikini kwenye kaya zao ilikuwa imekithiri na kuwafanya hali hiyo kuwakosesha elimu na huduma nyingine kwa watoto na wakashindwa kumudu kuzihudumia familia. Wakulima wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kudhamiria kuinua uchumi wa mtu wa kati kwa kutoa mbegu za tangawizi na vitendea kazi. Wanasema kukiwepo rasilimali ardhi, na watu wakipewa nyenzo Tanzania haitakuwa miongoni mwa nchi zinazolalamika na umasikini kwa kuwa mito ipo, maziwa yapo pamoja na mvua za kutosha. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Madaba, Vastus Mfikwa anasema, kwa kushirikiana na Mbunge wameweza kuzitembelea kata zote na kuainisha vipaumbele vya kuwakomboa wananchi kiuchumi kielimu na kiafya. Mfikwa anasema Mbunge ametoa mbegu tani sita za tangawizi, ameweza kugawa pikipiki 3 pamoja na baiskeli 6 kwa ajili ya walemavu na baiskeli nyingine kupeleka katika kituo cha afya Madaba ili iweze kusaidia wagonjwa wasiojiweza kutembea kutoka wodi moja hadi nyingine. Anasema, kwa muda mrefu Mbunge Mhagama amekuwa akishirikiana zaidi na wananchi kwa kuanzisha miradi kwa wakulima wadogo ikiwa ni pamoja na kilimo cha ufuta, alizeti na tangawizi hivyo ameahidi kushirikiana na madiwani wenzake kuhakikisha jimbo hilo linakua kwa kasi kiuchumi. Kwa mujibu wa Mfikwa, Halmashauri ya Madaba ina jimbo jipya na ina wananchi wenye vipato vidogo hivyo wanahitaji kujengewa uwezo zaidi ambao utamwezesha kila mwananchi ambaye ni mkulima kuwa na kipato kisichopungua Sh 300,000 kwa mwezi. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba, Robeti Mageni amewataka wadau wa maendeleo kujitokeza kwa wingi ili waweze kushirikiana kuipaisha kiuchumi wilaya hiyo. Anatoa changamoto kwa wazawa wa eneo hilo ambalo wapo ndani na nje kutumia fursa za kiuchumi zilizopo wilayani humo na wajitahidi kila moja kwa nafasi yake kuwezesha maisha yenye
agriculture
Tafadhali Share na marafiki story hiiagriculture
Tafadhali Share na marafiki story hiiKambale (Ietalurus Punetaus), ni aiana ya samaki ambao wana majina mengi kulingana na eneo na jamii husika. Samaki hawa unaweza kusikia wakitajwa kwa majina mengine kama vile, kambale channel, koleo, samaki kidevu n.k. Asili ya Kambale Asili ya samaki hawa ni Amerika ya Kaskazini. Samaki hawa hukua kwa haraka sana, na kuwa na uzito mkubwa. Aina hii ya samaki hupendwa na watu wengi kwa kuwa nyama yake ina ladha nzuri na ni laini sana. Samaki hawa huzaliana vizuri zaidi wanapokuwa mtoni au sehemu ambayo wanapata tope. Mfugaji anapokusudia kufuga aina hii ya samaki kibiashara, ni lazima kusakafia bwawa ili kuepuka uharibifu unaoweza kusababishwa na samaki hawa. Umbile lake Samaki aina ya kambale wana umbo refu, mpana kuanzia shingoni, ingawa kichwa ni kidogo, na upande wa mkia ni mwembamba. Samaki hawa wana rangi ya kijivu na wengine nyeusi. Jinsi ya kulisha kambale Unaweza kulisha kambale kwa kutumia unga wa samaki, maharagwe yaliyosagwa, mahindi, mchele pumba, ngano na bidhaa nyingine. Unaweza kujenga mfumo ambao utawawezesha samaki hawa kupata aina mbalimbali za wadudu, pamoja na majani, ili kusaidia wapate mlo kamili. Ukuaji na uvunaji wa kambale Aina hii ya samaki, wakitunzwa vizuri, wanaweza kukua kwa haraka na kuwa na uzito mzuri unaoweza kumpatia mfugaji faida nzuri. Unaweza kuanza kuvuna kambale baada ya miezi sita tangu walipopandikizwa kwenye bwawa. Soko la kambale Fikiria soko la samaki kabla ya kuanza kuzalisha. Wafugaji walio wengi, wamekuwa wakianzisha miradi ya ufugaji wa samaki kwa kufuata mkumbo bila kutambua kwanza soko watakalozalishia samaki hao. Jambo hili huwafanya wafugaji kuwa na kipato kidogo tofauti na nguvu waliyotumia kuzalisha. Inapofikia wakati wa kuvuna samaki, kiasi kikubwa huuzwa papo hapo bila kufika kwenye soko halisi, jambo linalosababisha kipato kuwa duni. Ni vyema mfugaji akawa na soko maalumu ambalo atazalishia. Unaweza kuzalisha kwa ajili ya shule, hospitali, vyuo, au taasisi yoyote. Halikadhalika jamii inayokuzunguka na taasisi nyinginezo. Mambo ya kuzingatia kabla ya kufuga samaki • Fahamu ni aina gani ya samaki inayopendwa zaidi katika eneo ulipo. • Samaki wanaopendwa wanatakiwa wawe na ukubwa gani. • Kiasi cha samaki kinachohitajika katika soko ulipo. • Ni kipindi gani ni kizuri kwa uvunaji wa samaki. • Ni wakati gani mzuri wa kuuza samaki. • Je, katika eneo lako kuna mfugaji mwingine anaezalisha samaki kwa ajili ya soko hilo?. • Bei ya aina ya samaki unaozalisha ikoje? Wasikilize wateja Wakati wote mfugaji anapouza samaki, ni lazima kusikiliza kwa umakini, wateja wako wanasemaje. • Je, wanapendelea samaki unaouza. • Je, samaki wako ni wadogo sana au ni wakubwa sana. • Wakija kununua wananunua kwa kiasi gani, kikubwa au kidogo. • Je, wanapendelea uzalishe zaidi? • Je, kuna wafanyabiashara wanataka uzalishe zaidi ili nao wanunue. • Wanataka samaki wawe kwenye ubora gani. • Wanaridhika na bei unayowauzia. Fuata haya kwa ufanisi wa soko la samaki • Hakikisha samaki wako katika hali ya usafi na vyombo salama unapovua tayari kwa kupeleka sokoni. • Samaki ni bidhaa inayoharibika kwa haraka, hivyo hakikisha unawapeleka sokoni mara tu baada ya kuwavua. • Hakikisha gharama za usafiri, utunzaji na uhifadhi, zinalipwa kutokana na bei ya soko. • Kumbuka gharama za uhifadhi wa bidhaa inayoharibika haraka kama samaki ni kubwa, hivyo vua kwa awamu kulingana na mahitaji. • Unaweza kuongeza thamani ya samaki kwa kufanya mambo ya msingi yanayohitajika kwenye uandaaji wa samaki, kama vile kuparua na kutumbua. • Unaweza kuwasafisha, na pia kuwakaanga kulingana na soko husika. Kwa kuzingatia mambo hayo machache, mfugaji anaweza kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuwekeza kwenye mradi wa ufugaji wa samaki. Pia ni muhimu kuzingatia mahitaji muhimu ya ufugaji wa samaki, ili kuepuka gharama zisizo za lazima. Tengeneza chakula cha samaki mwenyewe Mfugaji anaweza kupunguza gaharama za kununua chakula kwa ajili ya samaki, kwa kutengeneza chakula mwenyewe kwa kutumia malighafi ulizo nazo katika eneo lako. Tumia resheni rahisi ambayo itakupatia chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu. Mahitaji • Pumba ya mahindi sadolini 1. • Pumba ya ngano au mpunga sadolini 1. • Dagaa sadolini 1. • Kilo moja ya soya. • Robo kilo ya mashudu ya pamba au alizeti. Namna ya kuandaa • Changanya malighafi hizo kwa pamoja. • Saga hadi zilainike. • Kanda kama vile unga wa kutengenezea chapati. • Weka kwenye mashine ya kusaga nyama au kutengenezea tambi. • Anika kwenye jua la wastani. • Baada ya kukauka, vunja vunja kwenye vipande vidogo vidogo hasa kwa kuzingatia umri wa samaki unaokusudia kuwalisha. • Tumia lishe hiyo kwa samaki mara tatu kwa siku.
Recent Comments