education
Tafadhali Share na marafiki story hii🍹Morning Rise Up🍹
✍🏽```AJALI HAIKUKATISHA NDOTO YA WAKONTA👇👇 ```
Jana nikiwa nasikiliza taarifa ya habari *TBC1* katika kipindi cha *HADUBINI* nilikutana na jambo lilonisikitisha sana.Ni jambo lilomkuta Wakonta Kapunda ambaye alikuwa akisoma Masomo ya kidato cha sita mwaka 2012 katika shule ya sekondari ya wasichana ya Korogwe iliyoko mkoani Tanga .Kisa hiki ni cha kweli na iko hivi:
_Ilikuwa ni siku ya mahafari ya kumaliza kidato cha sita shule ya wasichana Korogwe *mwaka 2012*,kama ilivyo ada siku ya sherehe wanafunzi na hasa wahitimu hujawa na furaha tele ndivyo ilivyokuwa kwa wahitimu siku hiyo akiwemo Wakonta._
_Basi wakati wa shamrashamra za huku na kule kabla ya sherehe kuanza rasmi ,wahitimu walikuwa wakizunguka huku na kule wakisalimiana na ndugu na marafiki waliokuwa wamefika kwenye sherehe hiyo .Wakonta naye alikuwa akipeana mkono wa pongezi na ndugu zake huku akiwa amejawa na furaha tele ya kumaliza masomo ya kidato cha sita._
_Wakati shamrashamra hizo zikiendelea na Wakonta akiwa anaenda huku na kule ghafla mhitimu mmoja aliyekuwa akiendesha gari ambalo lilisemekana lilikuwa la mjomba wake alimgonga Wakonta na wakonta akaaumia sana huku shingo lake likivunjika na sehemu nyingi sana za mwili zikivunjika vibaya.Loo! Simanzi ,Vilio vilijaa na sherehe ile haikuwa sherehe tena kilio kikatawala kwa jambo lilokuwa limetokea na sherehe haikuweza kuendelea ,Wakonta akawa amekimbizwa Hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matabibu_.
_Ashukuriwe *Mungu* kuwa hakuna aliyepoteza maisha ingawa Wakonta alivunjika sana na baada ya matibabu hakuwa tena anaweza kufanya chochote kwa kutumia mikono wala miguu akawa ni mtu wa kufanyiwa kila kitu kwa kuwa viungo vyote vilikuwa vimelemaa.Mama yake mzazi na baba yake mzazi ndio wanamsaidia kufanya kila kitu._
_Hata hivyo Wakonta anasema kuwa pamoja na kupata ajari mbaya sana iliyomlemaza viungo hakukata tamaa na ndoto yake .Wakonta anatumia ulimi wake kutumia *IPAD* kuingia mtandaoni na kutafuta *taarifa* hasa za uandishi wa Script za Movie maana ndoto yake ni kuwa mwandishi mkubwa wa kuandaa senima na amekuwa akiandika mara kwa mara huku akipata taarifa na maarifa kupitia mtandao wa Internet.Nilishuhudia jana kupitia *TBC 1* Wakonta akiwa anatumia ulimi kwa ufundi mkubwa sana kuandika script hizo ambapo ulimi hugusa vitufe vya IPAD na kuandika .Ni kitu ambacho unaweza usiamini lakinii ndivyo ilivyo kuwa hutumia ulimi kuandaa sinema hizo na tayari ana kikundi cha kuigiza ambaye yeye anategemewa huko kwao ama kweli hujafa hujaumbika_ .
_Wakonta sasa baada ya serikali kumsikia,waziri wa habari mheshimiwa Nape Nauye alifika kwao kwa ajili ya kumsaidia na hasa kukuza kipaji chake alichonacho_
*TAFAKURI*
```📝Maisha yetu yako mikononi mwa Mungu .Mshukuru Mungu kwa kuwa hai leo .Kesho yetu hatuijui ni bora sana tukaishi leo kwa kufanya makubwa sana kadri ya uwezo wetu .Wakonta hakujua kitakachompata siku ile ya sherehe .
📝Wakonta ametoa somo kubwa kwamba pamoja na kuwa viungo vyake vimelemaa hakubweteka na kuona kuwa ndoto zake haziwezekani na sasa kwa kutokuficha kipaji chake serikali imemuona .Yawezekana wewe ni mzima na pengine huna hata ulemavu lakini umeficha uwezo wako hata sielewi ni sababu ipi ya msingi .Hujajiuliza kwanini wanapata ajari wengine siyo wewe??? Mbona siku ile unasafiri ilipotokea ajari alikufa mwingine siyo wewe???? .Anza kufanya unayoweza kufanya bila kusingizia chochote maana kama ni kisingizio Wakonta angekaa asifanye chochote na watu wakamsaidia . ```
Gospel
Tafadhali Share na marafiki story hiiUTAPELI KTK SIMU
Uungwana una gharama zake.
Dakika chache zilizopita amenipigia mtu simu. Ametumia namba 0764882284, akajitambulisha anaitwa Paul akipiga simu kutoka Vodacom Huduma kwa Wateja. Akaniambia kuwa kuna mtu amepiga simu kuwa amenitumia pesa kupitia Mpesa kwa makosa. Nikamwambia kuwa sijaona pesa yoyote ikiingia kwenye simu yangu.
Akaniambia kuwa wakati mwingine sms huchelewa kuingia kwa sababu za kimtandao. Kwa kuwa kila siku ninatumia huduma hiyo, akili yangu inayasadiki maelezo yake.
Akaniuliza kama ninakumbuka salio langu la mwisho. Kwa kuwa ninatumia sana hii huduma, ninafahamu salio langu. Ukizingatia tayari akili yangu iliwaza kuwa ninazungumza na mfanyakazi wa Vodacom, sikusita kumtajia kuwa kwenye akaunti yangu kuna 42,570/=
Akaniambia kama sms haijaingia nisubiri atanipigia pindi itakapoingia.
Wakati namaliza tu kuongea naye, napokea sms (kwa haraka haraka niliiona kama ya Mpesa) ikinionesha kuwa nimepokea kiasi cha shilingi 40,000/= kutoka namba 0759526921 iliyosajiliwa kwa jina la Daniel Oswald.
Wakati tu namaliza kuisoma hiyo sms napokea simu kwa yule bwana aliyejitambulisha kuwa anaitwa Paul akipiga simu kutoka Vodacom. Nikidhani ninazungumza na mtu wa Vodacom, na kwa uungwana kwa kuwa nimeona watu wengi wakipoteza pesa nyingi kwa kutuma kimakosa, ninamjibu kuwa nimeona hiyo text kuwa 40,000/= imeingia kwenye simu yangu.
Bwana Paul, kama alivyojitambulisha, akaniambia kwa kuwa system ya Vodacom ipo slow anaomba nimsaidie kuirudisha hiyo pesa kwenye namba 0759526921. Nikamwambia sawa hakuna tatizo nitafanya hivyo. Akaniambia nirudishe 39,000/= ili nisikatwe mie ada ya muamala.
Kwa kuwa akili yangu ilizingatia kuwa kweli kuna pesa imeingia, nilipokata tu simu sikurudi tena kwenye sms. Nikapiga * 150*00#. Nikatuma pesa kwenye hiyo namba ambayo nilikuwa tayari nimeinakili kwenye notebook yangu. Tena wakati natuma nilikuwa nikimwambia mtu niliyekuwa naye kuwa huwa naona huruma sana mtu akikosea kutuma pesa. Huwezi jua wakati mwingine ana shida kiasi gani. Wacha nifanye hima kumrejeshea.
Mpesa waliponiletea sms ya kukamilika kwa muamala naona salio langu limeshuka hadi elfu tatu na ushei.
Ndipo akili ikachangamka. Nikaenda kwenye sms ya nyuma na kugundua nimetapeliwa. Nikapiga Vodacom huduma kwa wateja. Nilipotoa maelezo, wakaniambia hiyo pesa tayari imekwishatolewa kwenye simu ya mhusika. Kwamba hawawezi kuwa na namna ya kunirejeshea. Chini ya dakika tatu ujue.
Nikamtumia text huyo bwana Paul (kama alivyojitambulisha) kuwa namshukuru sana kwa kunitapeli lakini 39,000/= itamwongezea tu umasikini, zaidi, umasikini wa fikra.
Halafu nikacheka tu. Nami leo nimepatikana. Ama kweli, ndege mjanja, lake tundu bovu.
Kwa nini nimetumia muda wangu kuyaandika haya? Sitaki nawe utapeliwe. Angalau, isiwe kizembe kama nilivyofanya mie.
Mchana mwema.
Fadhy Mtanga,
Mbeya.
Alhamisi, Septemba Mosi, 2016.
SHARE NA WENGINE WASIUMIZWE
social
Tafadhali Share na marafiki story hii🍹Morning Rise Up🍹
✏```HUPASWI KULA KILA KITU SAFARINI```
_Tulipokuwa stendi ya magari kabla ya kutoka *Ubungo* ,ndugu *Mla vyote* alinunua maji akijua yatamsaidia njiani .Tulivyokuwa tukiendelea na safari ndugu huyu alikuwa anatamani kununua kila kitu ambacho alikuwa analetewa dirishani asijue kama yuko safarini_
_Tulivyofika *Morogoro* mla vyote *alinunua chips* ili zimsaidie njiani kabla ya kufika sehemu ambapo angepata chakula cha mchana maana tulikuwa tuko mbali na Kitonga ambayo ilikuwa ndiyo g&sehemu ambapo tungepata Chakula._
_Alivyokula zile chips ndugu huyu hakujua kuwa zile chips zilikuwa zimechacha na mara tu baada ya kula chips tumbo lake likaanza kusumbua na safari yake ikaanza kuwa mbaya .Hakuwa tena ana furaha ya safari ile kwa kuwa kila muda tumbo la kuhara lilikuwa linamsumbua. *Loo!* Mla vyote Alipata shida sana na hasa ukizingatia kuwa basi lilikuwa halina choo Nilimuonea huruma sana lakini sikuwa na jinsi ya kumsaidia zaidi ya kumpa pole na kufanya jitahada za kutafuta namna ya kutuliza tumbo lake lilokuwa likimuuma sana_
_Mla vyote aliniambia kuwa sasa amaejifunza kutokurupuka kula vitu njiani wakati anasafari kwa kuwa safari siyo sherehe ._
*TAFAKURI*
📝```Maisha ni safari ndefu inayohitaji umakini mkubwa sana .Wakati uko njiani utakutana na watu wengi ambao wanaweza kukudhuru na usiendelee na safari au kutofurahia safari yako.Watu wa namna hii unapaswa kukaa nao mbali huku ukiweka pamba masikioni kutosikiliza yale wanayoyasema .
📝Maneno ya kukatisha tamaa ni moja ya vyakula vyenye sumu na vilivyochacha ambavyo vitasababisha uone safari yako kuwa chungu .Njiani wakati unaendelea na hatua za ndoto yako utakutana na mambo ambayo unaweza kufikiri kuwa vitakusaidia kukufikisha kwenye hatma ya ndoto zako kumbe vinaua ndoto zako.
📝Achana kabisa na vitu ambavyo havina tija katika safari yako ya kufika pale unapotaka kufika .Sikia siyo lazima kuzingatia kila ushauri unaopewa na watu maana unaweza kukudhuru kama Mla vyote aliyodhurika na chips alizokuwa amenunua akidhani kama zingemsaidia .
📝Iko hivi Mpendwa,utakaporuhusu kila kitu kuingia masikioni mwako na kwenye ubongo wako kuna wakati ubongo wako utajaa sumu na utaona kila kitu hakiwezekani .
Wakati mwingine nikiwa nafundisha hatua tano za kufikia mafanikio kwenye Kijana Jithamini niliwaambia kuwa ubongo wa mwanadamu ni kama glasi yenye maji ambayo maji hayo mtu akiweka sukari maji hayo yatakuwa matamu ,lakini maji hayo hayo mtu akiweka sumu ,ukinywa utakufa```
social
Tafadhali Share na marafiki story hiiTABIA MBAYA KUMI ZINAZOFANYA USHINDWE KUWA NA AKIBA "SAVINGS"....HATIMAE UNAKOSA MTAJI WA KUFANYA MAMBO YAKO...
1.Unanunua nguo bila mpangilio..
Kuna watu wana nguo kama duka. Plz Kuwa na nguo chache Tu huwezi kushindana na fashion.
2.Unanunua Viatu bila mpango.
Viatu pia vinameza savings zetu. Nunua pea chache zenye ubora ili zidumu.
3.Unatoa ofa bar bila mpango.
Nenda bar kwa bajeti mahususi. Hakuna atakae kusifia kwa kutoa ofa hovyo. Kila mbuzi ale kwa urefu Wa kamba yake. Jifunze ubepari.
4.Unatumia hela nyingi kwenye simu ambazo sio productive. Unaweka vifurushi vya week vya sh 7000 au 10000 ili uchati na marafiki Fb au wasaap Huo ni ujinga. Badilika.
5.Unakopa hela benki na kununua vitu kama simu ya milioni na gari ambazo sio productive. Unakosa hela hata ya mafuta, gari la nini kwanini usingewekeza sehemu ili kuwe na mradi Wa kuzalisha ndio ununue gari?
6.Una marafiki wengi ambao ni mizigo kwako au hamuendani kivipato hivyo unajikuta unalazimika kutumia zaidi ya kipato chako ili uwa-impress. Meneja Wa TRA na mwalimu Wa sec unatarajia utoe offer mpaka umfurahishe meneja? Utabaki na sh ngapi toka kwenye salary yako?? Zinduka.
7.Huna timetable ya kudumu ya maisha yako, unajikuta unaburuzwa Tu na marafiki zako kwa kwenda sehemu mbalimbali za matumizi.
Kuwa na ratiba za maisha yako na zisimamie kikamilifu, usiburuzwe!
8.Una michepuko inayokutegemea wewe kwa kila kitu. Wanakuita ATM we we unakenua Tu huzinduki. Badilika.
9.Una huruma sana kuliko kipato chako. Yaani kila ukiombwa unatoa hata kama muombaji hana genuine need. Usiwe mkristo kuliko Yesu. Fanya hivyo kama ni lazima. Ila sio kila anaekupiga mzinga unapigika.
10.Unatembea na hela nyingi kwenye wallet au mshahara wote kwenye wallet au handbag au nyumbani kwako. Unapokuwa na petty cash nyingi unatengeneza mazingira ya kutumia hovyo. Jifunze kuweka hela benki. Tembea na hela Tu unayoihitaji kwa matumizi ya lazima.
Naamini tukizingatia kanuni hizi kumi tutaongeza savings zetu na kuwa na mtaji Wa kufanya vitu vikubwa endelevu
😳😳😳😳😳😳😳.
Life Style
Tafadhali Share na marafiki story hii*SABABU ZA MAGOJWA YA FIGO. JIHADHARI NA ONYEKA!.*
Raia wa Ghana wanazidi kufa kwa matokeo ya ugonjwa wa Figo.
*JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:*
*1.Usichelewe kwenda HAJA.* Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo baya. Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu. Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu huzidisha bakteria haraka.
Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha maambukizi ya figo, pia njia ya mkojo na "nephritis", pamoja na "uremia". Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo.
*2. Kula Chumvi kupita kiasi.* Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa siku.
*3. Kula nyama kupita kiasi.*
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa Protini unazalisha amonia- sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi inaleta uharibifu zaidi wa figo.
4. *Unywaji mwingi wa "Caffeins".*
Caffein hutokana na vinywaji vya Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redblue n.k. Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza mateso. Unapaswa kupunguza kiwango cha Coke, Pepsi, Red Bull, nk ambavyo hunywa kila siku.
*5. Kutokunywa maji.*
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri. Endapo hatunywi ya kutosha, sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu, kama hakuna kimiminika cha kutosha kutoa kwa njia ya figo. *** Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku.
Kuna njia rahisi ya kuangalia kama unakunywa maji ya kutosha: Angalia rangi ya mkojo wako; Wepesi wa rangi, ndiyo vzuri.
*6. Kuchelewa matibabu.*
Tibu matatizo yako yote ya kiafya kwa uhakika na uwe unachunguza afya yako mara kwa mara. Wapendwa na wapenzi wangu, hebu tujisaidie wenyewe... Shirikisha wengine, kama unajali. ----------------
*Pia epuka vidonge hivi, ni hatari sana:*
D- baridi*
Vicks Action- 500*
Actified*
Coldarin*
Cosome*
Nice*
Nimulid*
Cetrizet- D
Hivi vidonge vina Phenyl propanol- amide PPA ambayo husababisha stroke na ni marufuku Marekani.
MWISHO... Tafadhali, kabla ya kufuta, msaidie rafiki yako kwa kumpitishia hii..!
*Inaweza kumsaidia mtu!*
Wasambazie wengi kwa kadiri uwezavyo.
Shirikisha ujumbe huu kwa mpendwa wako.
*Maonyo muhimu ya Afya*
1. Jibu (pokea) simu wito na sikio la kushoto.
2. Usinywe dawa zako kwa maji baridi....
3. Usile milo mizito baada ya saa 11 jioni.
4. Kunywa maji vuguvugu mengi asubuhi na kiasi usiku. Usinywe maji baridi kamwe.
5. Muda bora wa kulala ni kutoka saa 4 usiku hadi saa 10 Alfajiri.
6. Usilale mapema baada ya kumeza dawa au baada ya mlo. Usiku, Kula chakula laini.
7. Usipokee simu yako ikiwa haina chaji. Wakati huo mionzi huwa ina nguvu mara 1000 .
Je, unaweza kuwasambazia watu unao wajali?
Mimi nimeshafanya kwako....!!.
Health
Tafadhali Share na marafiki story hii```"MTAJI WAZO VS MTAJI FEDHA "
Swala la nini kinapaswa kuwa cha kwanza kati ya *mtaji wa fedha na wazo la kibiashara* limewatatiza wengi sawa na shairi lile la darasa la tano liliouliza *"YAI AU KUKU NANI KATANGULIA?"*.
✍🏽Uhalisia ni kwamba hata fedha yenyewe ni wazo na kimsingi kitu chochote cha kushikika kilitokana na wazo fulani na badae wazo hilo likawekwa katika uhalisia.
Siku moja nilikuwa naongea na watu fulani nikawaambia kwamba siku zote mtaji fedha hufuata mtaji wazo .Yapo mawazo ambayo yanakupa mbinu za kupata fedha hivyo basi tatizo kubwa tusiseme ni mtaji fedha lakini wengi tuna tatizo la kukosa mtaji wazo.
📝Ukweli ni kwamba watu wengi hatuna mawazo .Kwa mujibu wa mwandishi wa vitabu,mhamasishaji na mwanzilishi wa makanisa ya winners chappel Pator David Oyedepo anasema “``` 5% ya watu wote duniani ndio wenye mawazo, 15% ya watu wanadhani kuwa wanawaza kumbe hawawazi na 80% ya watu wote duniani wanakufa bila kuwaza”(hii ni hatari).```
Napoleon Hill aliwahi kuuliza swali hili ```"if you get a million dollar what will you do???"```. Napoleon Hill alitambua kuwa binadamu wengi wanalamika hawana fedha huku wakiwa hawana mawazo ya nini watafanya baada ya kupata fedha .Wewe ni shahidi umekuwa ukipata pesa mara ngapi na umezifanyia nini??(unajua mwenyewe).
Watu wengi wana fedha lakini hawana mawazo sasa kwako wewe hii ni fursa ya kutumia mtaji wazo kupata hizi fedha ambazo hazina kazi zimekaa tu .Shida wengi hatutaki kuumiza vichwa na kuzalisha mawazo yenye tija *(productive ideas)*.Kama wewe una sh laki moja na unahitaji kuanza biashara ya laki sita na huna fedha hiyo kwanini usiungane na marafiki wazuri 6 ulionao wenye uwezo wa kupata laki moja kwa mwezi mkafanya mchezo na ukapata hiyo pesa kiulaini???(umekosa mawazo siyo mtaji).
📝Kuna watu hapa mjini ni *madalali* wa mambo lukuki na wanapata hela sana bila kutumia hata chembe ya shillingi .Fikiria dalali anapangisha watu watano au kumi kwa mwezi anapata sh ngapi ?? bado dalali huyu huyu yuko kwenye viwanja, kumbi n.k .Mtu huyu anapata pesa nyingi .
Kuwa dalali siyo kwamba hujasoma , acha mawazo potofu .Dalali ni *Third part* anayekurahisishia kupata huduma uitakayo haraka hata wewe unaweza kuamua kuwa dalali na ukaendelea na maisha (tumekuwa vipofu)
📝Acha kabisa kulalamika kuwa huna mtaji wakati huo una simu ya laki saba na unaweka vifurushi vya elfu moja kila siku na kupanda bodaboda kila siku na hujui kwa mwaka unatumia kiasi kikubwa kiasi gani huku ukisema huna mtaji wa laki mbili kuanzisha biashara
```Akili yako ,Maisha yako```
Recent Comments